Abel mutua asimulia alivyombusu Sarah Hassan

Muunda maudhui huyo ameelezea jinsi alivyompiga busu Sarah Hassan wakati wa maigizo hapo awali.

Muhtasari

•Mwigizaji wa Kenya Sarah Hassan, ambaye aliwahi kuigiza pamoja na Abel Mutua enzi hizo katika kipindi cha 'Tahidi High' kilichokuwa kikionyeshwa kwenye runinga ya Citizen kama 'Tanya', alitajwa kuwa mwigizaji mpole sana.

•Sehemu ya pili ya mwisho wa kipindi changu katika kipindi nilimpiga mate mbaya kwa class.

Sarah Hassan na Abel Mutua
Image: Istagram

Mwigizaji  kutoka Kenya Abel Mutua, maarufu kwa mashabiki wake kama ‘Mkurugenzi’, alisimulia jinsi alivyoishia kumbusu mwigizaji Sarah Hassan.

Akizungumza katika mahojiano na Mic Check Podcast, Abel Mutua alikiri kumbusu mwigizaji huyo wa Kenya wakati wa  wakiigiza.

“Tanya  yaani Saraha Hassan alikuwa mpolite lakini Mungu ni nani kipindi chetu cha mwisho kabisa nikasema walahi huyu dem huyu vile amekua akininyima.

Sehemu ya pili ya mwisho wa kipindi changu  nilimpiga mate mbaya kwa class.” Abel Mutua alifichua.

Mwigizaji wa Kenya Sarah Hassan, ambaye aliwahi kuigiza pamoja na Abel Mutua enzi hizo katika kipindi cha 'Tahidi High' kilichokuwa kikionyeshwa kwenye runinga ya Citizen kama 'Tanya', alitajwa kuwa mwigizaji mpole sana.

Abel alikuwa sehemu ya uandishi wa kipindi hicho, alihakikisha kwamba alikuwa na njia yake na mwigizaji huyo, akikiri kwamba ni wakati ambao alifurahia kikamilifu.

Abel alisema kuwa ni katika onyesho yao ambapo kulikuwa na sehemu ya kipindi ilikuwa lazima tukio hilo lifanyike.

“Mungu ni nani. Sasa unakataa na script ndio imesema” Abel Mutua alifichua wazi, akionyesha furaha yake.