Kanyari adai wanawake wanaotumia iPhones na kuongea kizungu si 'wife materials'

Baada ya kejeli hizo Kanyari hakulaza damu bali aliomba msamaha.

Muhtasari
  • Alifanya hivi kwenye ukurasa wake maarufu waTikTok ambapo alianza kwa kusema kuwa wanawake wanaozungumza Kiingereza sio wake na hawawezi kuwa wake wazuri.

Pasta Victor Kanyari amewasisimua Wakenya kwa mara nyingine baada ya kutoa maoni yenye utata kuhusu aina ya wanawake ambao si wazuri katika kuwa wake.

Alifanya hivi kwenye ukurasa wake maarufu waTikTok ambapo alianza kwa kusema kuwa wanawake wanaozungumza Kiingereza sio wake na hawawezi kuwa wake wazuri.

"Kubali ukatae! Wife material haongeangi kizungu. Kama naongea uongo niambie! Nakama naongea ukweli andika hapo kwa comments, 'Prophet uko on point,'" alisema kwa imani kubwa.

Kabla ya kuendelea kurudia tena, “Wife Material haongeangi kizungu.

Kisha akaendelea kuwakasirisha watumiaji wa iPhone, kwa kusema,

"Wife material hatumiangi iPhone! Anatumia katululu. Ukiona msichana anatumia iPhone, jua huyo siyo wife material."

Kama ilivyo kwa mambo mengi ambayo kasisi husema na kufanya kwenye TikTok, kauli yake pia ilivutia mashabiki wengi huku wengine wakikubaliana naye na kuwaacha wengine wakipigwa na butwaa.

Kanyari amekuwa akigonga vichwa vya habari siku za jivi majuzi baada ya kupokea zawadi ya kondomu kutoka kwa mfuasi wake wa Tiktok madhabahuni.

Wakenya na wanamitandao walijitokeza na kumuonya Kanyari akome kumdharau Mungu kwenye madhabahu yake.

Baada ya kejeli hizo Kanyari hakulaza damu bali aliomba msamaha.