Kitinda-mimba amlilia boyfriend wake kumuoa haraka ili kumuokoa dhidi ya kuendelea na masomo

Mwanafunzi huyo wa masomo ya baada ya sekondari alimsihi mpenzi wake kufanya haraka ili kufika kwao na kumlipia mahari kama njia moja ya kuhakikisha amemnasua kutoka kwa ‘janga’ la kuendelea na masomo.

Muhtasari

• Kwa mujibu wake, kuendelea na masomo ni jambo gumu sana na ambalo hawezi kulikwepa isipokuwa tu kuitorokea ndoa.

Image: screengrab

Ni hadithi zipi ambazo unazisikia zinahusishwa na watoto haswa wale wa kike ambao ndio vitinda mimba katika familia zao?

Kijana mmoja katika mtandao wa TikTok ameshiriki uzoefu wake kutokana na kuchumbiana na mwanamke ambaye ndiye kitinda mimba kwao.

Kijana huyo alipakia video wakiwa na mpenzi huyo wake ambaye ni kitinda mimba katika familia yao, na kuonyesha jinsi anataabika kumlea kimapenzi, akilazimika kumhendo kwa utaratibu na umakini mkubwa kama yai ili asije akamkera na kumuudhi.

Kwa kawaida, watoto vitinda mimba katika familia hudekezwa kwa mtindo wa kipekee, muda wote wakichukuliwa kuwa na akili za kitoto hata kama wameshakomaa na kuwa watu wazima.

Katika video hiyo, mrembo huyo ambaye kwa muonekano ni mwanafunzi wa masomo ya baada ya sekondari alionekana akimuomba na kumsihi mpenzi wake kufanya haraka ili kufika kwao na kumlipia mahari kama njia moja ya kuhakikisha amemnasua kutoka kwa ‘janga’ la kuendelea na masomo.

Kwa mujibu wake, kuendelea na masomo ni jambo gumu sana na ambalo hawezi kulikwepa isipokuwa tu kuitorokea ndoa.

Katika sehemu ya video hiyo, mwanadada huyo alionekana akiwa na wakati mzuri zaidi tofauti na alipokuwa akitokwa na machozi katika sehemu nyingine kuhusu kurejea shuleni.

"Njoo ulipe malipo kwa wazazi wangu ili nisiende shule tena," alisema.

 

Tazama video hapa chini…