Huddah ajibu kuhusu kuvumilia mshahara wa mbunge Salasya wa Sh2,000

Huddah alidokeza kuwa kiasi hicho hakitoshi na akabainisha kuwa mbunge huyo atahitaji kuchukua mkopo.

Muhtasari

•Shabiki mmoja alimuuliza ikiwa yuko tayari kustahimili Sh2000 ambazo Salasya anaenda nazo nyumbani kila mwezi baada ya kukatwa.

•"Itabidi akope mkopo," alisema.

HUDDAH NA SALASYA
HUDDAH NA SALASYA
Image: HISANI

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya lazima achukue mkopo ikiwa atachumbiana na crush wake Huddah Monroe, sosholaiti huyo mrembo amesema.

Huddah aliwashiriki mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram mnamo Jumatatu ambapo mfuasi mmoja alimuuliza ikiwa yuko tayari kustahimili Sh2000 ambazo Salasya anaenda nazo nyumbani kila mwezi mmoja baada ya kukatwa.

“Utavumilia hiyo payslip ya 2k ya mhesh, ama unawezamreplace na mimi, yangu ni 10k,” mtumiaji wa Instagram alimuuliza Huddah.

Katika majibu yake, sosholaiti huyo mrembo alidokeza kuwa kiasi hicho hakitoshi na akabainisha kuwa mbunge huyo atahitaji kuchukua mkopo.

"Itabidi akope mkopo," alisema.

Kutoka mshahara wa zaidi ya Sh1.1 milioni ambao Mbunge wa Mumias Peter Salasya alipokea mwezi wa Juni, alienda nyumbani na Sh2,364.

Hili lilithibitishwa na risiti ya mshahara ambayo mbunge huyo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook mapema Julai.

"Hii ndio salary yangu. Kama yangu inakaa hivi, ya askari mwalimu na daktari zinakaa aje?" Salasya alisema.

Kwenye kipindi cha Jumatatu, Huddah pia alizungumzia uwezekano wa kukubali kuolewa na mbunge huyo wa Mumias Mashariki.

Kutokana na kutaniana kati yake na Salasya ambako kumejiri katika siku za hivi karibuni, mashabiki wengi walimrushia maswali wakitaka kubaini uhusiano wake na mbunge huyo mcheshi na kama atamkubalia kuwa mpenzi wake endapo atapata nafasi kama hiyo.

“Unaweza kubali kuolewa na Salasya,” mmoja alimuuliza.

Akijibu, Huddah alimsifia Salasya kama mtu mcheshi muda wote na kusema kwamba hatojali kuwa mke wake.

“Ni mtu wa ajabu sana, anapenda kucheka muda wote. Ni mtu mwenye furaha saa ishirini na nne kwa wiki, mbona nisikubaliu,” Huddah alijibu.

Kuhusu kumvunja moyo, Huddah alisema kwamba hawezi fikiria hata ku8mvunja moyo kwa sababu anavyomjua mbunge huyo, hatostahimili.

Hivi majuzi, mbunge huyo alidokeza kwamba alikuwa katika awamu ya lala salama kujiandaa kukutana na Huddah lakini akaomba mashabiki wake usauri jinsi ya kukutana na mwanasosholaiti huyo ghali.

Wiki moja iliyopita, Huddah alikuwa amempa Salasya masharti kadhaa ya kukidhi iwapo alikuwa anataka kumpa mwaliko wa kukutana.

“Also sitaki story ya isukuti kwa airport. niko faragha. Naingiaga na ninja meeting zangu ni JW Marriott. Chumba cha rais… kimejaa waridi za machungwa. Salama na dola 30,000 za salamu ama sitaongea muda wote,” alisema.