Agundua yeye si baba wa mwanawe miezi 2 baada ya kusherehekea kuzaliwa kwake mtandaoni

Kwa sauti ya kuvunjika moyo, alisema kwamba amegundua mtoto si wake na kuwashauri wanaume kuendelea kuwa watu bora kwa kutenda wema japo wao wanatendewa mabaya.

Muhtasari

• Hata hivyo, miezi miwili baadae, Furquan amerejea tena kwenye mtandao huo akiwa na taarifa za kuvunja moyo kwamba amegundua binti huyo si wake baada ya kufanya vipimo vya msimbojeni, DNA.

Image: x

Mwanamume mmoja amevutia huruma katika mtandao wa X baada ya kuchapisha sasisho kuhusu kuzaliwa kwa mwanawe.

Mwanamume huyo kwa jina Furquan, miezi miwili zilizopita alichapisha kwa furaha kuhusu kuzaliwa kwa mwanawe wa kike, akiambatanisha na picha akiwa amempakata kwa furaha katika hospitali.

Hata hivyo, miezi miwili baadae, Furquan amerejea tena kwenye mtandao huo akiwa na taarifa za kuvunja moyo kwamba amegundua binti huyo si wake baada ya kufanya vipimo vya msimbojeni, DNA.

Hata hivyo, baada ya baadhi ya watu kumcheka, mwanamume huyo alifuta chapisho hilo, lakini kunao baadhi walikuwa tayari wamenasa picha ya chapisho lake akithibitisha kwamba amegundua yeye si baba mtoto.

Kwa sauti ya kuvunjika moyo, alisema kwamba amegundua mtoto si wake na kuwashauri wanaume kuendelea kuwa watu bora kwa kutenda wema japo wao wanatendewa mabaya.

Aliandika, "Yeye si wangu. Mpira juu juu 🚶🏾. I hate hii shit popped lakini Iont got mtawa kusema. Endelea tu kuwa mtu bora na uwatendee watu jinsi unavyotaka kutendewa. Kill em w Wema”.

x
x

Katika picha hiyo ya awali, mwanamume huyo alionekana akiwa amevalia gauni la kujifungulia akionyesha kuwa alikuwa chumbani na mpenzi wake kipenzi ambapo alimpokea mtoto huyo.

Alinukuu picha hiyo, "Wakati bora zaidi wa maisha yangu niliorekodiwa kwa wakati mwafaka".

Hili hapa chapisho la awali;