Jamaa alazimika kunyoa ndevu siku ya harusi yake baada ya pasta kudinda kufungisha ndoa

“Nilitolewa kanisani kwa sababu ya ndevu zangu siku ya harusi yangu. Wakati nilipotolewa kanisani kwa sababu ya ndevu zangu. Kasisi alisema hatafungisha ndoa yetu ikiwa sitanyoa ndevu zangu."

Muhtasari

• Kwa mujibu wake, alifika kanisani siku ya harusi akiwa na furaha lakini mchungaji akamfukuza kanisani akimtaarifu kwamba hangeweza kuifungisha harusi yake akiwa na shungi hilo la ndevu.

• Kadiri video inavyoendelea kuenea mtandaoni, watu wengi wamefurika sehemu ya maoni ili kushiriki mawazo yao kuhusu uamuzi wa kanisa.

BWANA HARUSI KUNYOA NDEVU.
BWANA HARUSI KUNYOA NDEVU.
Image: HISANI

Bwana harusi mmoja amezua vichekesho katika mtandao wa kijamii baada ya kusimulia kilichotokea siku ya kufungwa kwa harusi yake kanisani.

Kupitia video kwenye TikTok, jamaa huyo mwenye shungi la ndevu alieleza kwamba ndevu hizo zilikaribia kuiponza siku yake ku kanisani baada ya kumkorofisha na mchungaji aliyesimamia harusi yake.

Kwa mujibu wake, alifika kanisani siku ya harusi akiwa na furaha lakini mchungaji akamfukuza kanisani akimtaarifu kwamba hangeweza kuifungisha harusi yake akiwa na shungi hilo la ndevu.

Ilimbidi jamaa huyo kuchukua maamuzi ya haraka na kutafuta kinyozi wa karibu ili kumpa huduma ya kupunguza urefu wa ndevu zake na kuinusuru siku yake ya ndoa.

Katika video hiyo, alionekana akihudumiwa na kinyozi wa mtaani ambaye alifanya kupunguza ndevu zake kabla ya kuharakisha kurudi kanisani kwa ajili ya shughuli yake.

Katika chapisho, uso wa mwanamume unaonyeshwa na nukuu inayoelezea hali hiyo.

Maneno hayo yanasema: “Nilitolewa kanisani kwa sababu ya ndevu zangu siku ya harusi yangu. Wakati nilipotolewa kanisani kwa sababu ya ndevu zangu. Kasisi alisema hatafungisha ndoa yetu ikiwa sitanyoa ndevu zangu,” anaonyesha mwanamume huyo na mwanamume wake bora wakiwa wameketi kwenye gari.

Kadiri video inavyoendelea kuenea mtandaoni, watu wengi wamefurika sehemu ya maoni ili kushiriki mawazo yao kuhusu uamuzi wa kanisa.

Tazama baadhi ya maoni hapa chini:

PIKITO661: “Baadhi ya makanisa pia yana uasi. nikifanya harusi ya kortini nitaenda kufanya mapokezi bora zaidi jioni na marafiki na wanafamilia wachache. Sipati nguvu kwa ajili ya vurugu za kanisa.”

Palblackdiamond: "Je, hawakukuona wakati wa ushauri nasaha ili kukuambia kuhusu hilo?"

odinakaifeoma: “Ikiwa mimi ni mke hakuna mtu ambaye hatamtoa mume wangu kanisani kwa sababu ya ndevu zake wanapaswa kuzingatia kumwambia awe mume na baba asiye na ubinafsi na anayejali sura yake haifai.”

Tazama video hiyo hapa;