Huddah atoa onyo kali kwa wanaommezea mate baada ya Salasya kushindwa kumtongoza

"Nipende kwa hiari yako mwenyewe. Mimi ni vybz tuu & Inshallah,” Huddah alisema.

Muhtasari

•Hisia hizi zake zinakuja baada ya jaribio lisilofaulu la mwanasiasa Peter Salasya la kumtongoza katika wiki za hivi majuzi.

•Mrembo huyo pia alionekana kushangaa kwa nini mtu ajikite katika kumpenda ilhali hata hawajaonana naye.

HUDDAH NA SALASYA
HUDDAH NA SALASYA
Image: HISANI

Mwanasosholaiti mrembo kutoka Kenya Huddah Monroe amewaonya watu kuhusu hatari ya kumpenda.

Hisia hizi zake zinakuja baada ya jaribio lisilofaulu la mwanasiasa kijana Peter Salasya la kumtongoza katika wiki za hivi majuzi.

Katika taarifa ya Jumatatu, mjasiriamali huyo wa vipodozi alionya kwamba watu wanapaswa kumpenda tu kwa hiari yao wenyewe akidokeza kwamba mapenzi sio mambo yake.  

"Nipende kwa hiari yako mwenyewe. Mimi ni vybz tuu & Inshallah,” Huddah alisema.

Mrembo huyo pia alionekana kushangaa kwa nini mtu ajikite katika kumpenda ilhali hata hawajaonana naye.

“Subiri, unaingiaje hata kumpenda mtu ambaye hujawahi kukutana naye. Vumbi ni mara kwa mara. Kivumbi 2024,” alisema.

Haya yanajiri wakati sosholaiti huyo akionekana kuwa na mzozo wa mtandaoni na Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya ambaye amekuwa akianya juhudi za kumtongoza.

Hapo awali, Huddah alikuwa amemjibu mbunge Salasya akimbainisha kuwa yeye sio kienyeji.

Salasya alikuwa amezamia kwenye mitandao ya kijamii akitangaza kwamba amekata tamaa kuendelea kujaribu kumtongoza Huddah.

Salasya alisema kuwa hawezani na Huddah akidai kwamba kuna mambo yangeharibika.

"Mimi siwezani wataangusha serikali afadhali nirudi kwa vienyeji yangu. Najitenga rasmi kumfuata huyo msichana,"  Alisema Salasya.

Huku akimjibu Salasya, Huddah Monroe alimshauri Salasya kutamfuta mpenzi mwenye ni wa kiwango chake.Vile vile amemwambia kuwa yeye si kienyeji.

Mwanasosholaiti huyo alidai kwamba alikuwa ametumiwa shilingi milioni mbili na mtu ambaye hakuweka jina lake wazi.

Kulingana na Huddah, hangeweza kugundua ikiwa shilingi elfu kumi ziliingia kwenye akaunti yake kutoka kwa Salasya.

"Hakika ningewezaje kugundua shilingi 10,000! Hata sikugundua, sikuona ata,"  Alisema Huddah Monroe.

Hata hivyo, Huddah Monroe alimtaka Peter Salasya awache kumharibia jina kwa sababu ya pesa ambayo ni kidogo kwake.

Aidha, aliweka wazi kwamba alimrudishia Mbunge Peter Salasya pesa ambazo alikuwa ametumia kwake.