Akothee amuonya mumewe Omosh baada ya kutaka washiriki mapenzi kwenye stairs

“Mpenzi, kuna CCTV hapa. Kwa nini kwenye ngazi? Unaweza kusubiri,” Akothee alimwambia mumewe.

Muhtasari

•Kwenye video, mama huyo wa watoto watano alionekana akiwa amelala kwenye ngazi huku Bw Omosh akicheza juu yake

•Katika majibu yake, Omosh alimsihi mama huyo wa watoto watano waelekee chumbani mwao ili wamalize alichoanza.

wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Akothee na mumewe Denis Shweizer wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Siku ya Jumapili, mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee alichapisha video yake na mumewe Denis ‘Omosh’ Shweizer wakifurahia nyakati za kimapenzi kwenye ngazi (stairs) za jumba lao la kifahari.

Katika video aliyoweka kwenye Instastori zake, mama huyo wa watoto watano alionekana akiwa amelala kwenye ngazi huku Bw Omosh akicheza juu yake.

Mzungu huyo mzaliwa wa Uswizi alionekana wazi kuwa na hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mwanamuziki huyo alisikika akimuonya baada ya kugundua alichotaka.

“Mpenzi, kuna CCTV hapa. Kwa nini kwenye ngazi? Unaweza kusubiri,” Akothee ambaye alionekana kushangazwa na tabia ya mumewe alisikika akimwambia.

Katika majibu yake, Omosh alimsihi mama huyo wa watoto watano waelekee chumbani mwao ili wamalize alichoanza.

Akothee hata hivyo alikataa ombi la mumewe na kumwomba kwanza ampeleke shambani kabla waelekee chumbani.

“Kwanza tunakwenda shambani. Sitaahidi chochote, tutalala. Tunaenda shambani na kuona kile ambacho wafanyikazi wamefanya,” Akothee alisikika akisema.

Wanandoa hao walionekana wakibusiana mara kwa mara huku mwimbaji huyo akirekodi video kwa mkono wake mmoja.

Omosh alionekana kusisitiza wazo la kuwa na wakati wa kimapenzi na mkewe ambaye alisikika akilalamika kwa kejeli kwamba alichokuwa akimfanyia ni unyanyasaji wa kijinsia na kimapenzi (SGBV).

"Unajua hii ni SGBV," Akothee alimwambia mumewe.

Kufuatia malalamiko hayo, mzungu huyo aliinuka mara moja na kujitetea dhidi ya tuhuma hizo.

Akothee na  mumewe Denis Shweizer walifunga pingu za maisha katika harusi ya kifahari iliyofanyika Windsor Golf Hotel & Country Club, Nairobi mnamo Aprili 10, 2023.

Harusi hiyo ya pili ya mwanamuziki huyo ilipambwa na wanafamilia kadhaa, marafiki wa karibu, wasanii na wanasiasa mashuhuri nchini. Jumla ya watu wasiopungua 300 walialikwa kwenye hafla hiyo ya kufana.

Wawili hao tayari wametangaza kuhusu harusi ya pili ambayo itafanyika katika nchi ya asili ya Bw Omosh, Uswizi baadaye mwaka huu.