"Angekuwa ameniua" Akothee afunguka changamoto za kushirikiana malezi na baba mwanawe wa 4

Alifichua kwamba mzazi mwenzake wa mwisho, Dominic Decherf, ndiye huwa mpatanishi kila mambo yanapoharibika.

Muhtasari

•Akothee alijawa na bashasha siku ya Alhamisi jioni alipokuwa akiwakaribisha wanawe wawili, Prince Oyoo na Prince Ojwang, nchini Kenya.

•Alizungumzia changamoto za kushirikiana katika malezi akidokeza kuwa haijakuwa rahisi na mzazi mwenzake wa pili, Bw Markus almaarufu Papa Ojwang.

Akothee, Papa Ojwang pamoja na watoto wake wawili
Image: HISANI

Mwanamuziki Esther Akoth almaarufu Akothee alijawa na bashasha siku ya Alhamisi jioni alipokuwa akiwakaribisha wanawe wawili, Prince Oyoo na Prince Ojwang, nchini Kenya.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 aliwapokea wavulana hao wawili ambao wamekuwa wakiishi Ufaransa na mzazi mwenzake wa mwisho,  Bw Dominic Decherf,  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na hakuweza kuficha furaha yake alipowatazama wakiwasili kwenye eneo la kusubiri abiria.

"Watoto wamefika, wacha sherehe ianze," Akothee alisema chini ya video yake akiwapokea wanawe ambayo aliichapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Mama huyo wa watoto watano aliendelea zaidi kuzungumzia changamoto za kushirikiana katika malezi akidokeza kuwa haijakuwa rahisi na mzazi mwenzake wa pili, Bw Markus almaarufu Papa Ojwang ambaye anatoka Uswizi.

Katika taarifa yake, alidokeza kuhusu ukaidi wa mzungu huyo wa Uswizi akifichua kwamba mzazi mwenzake wa mwisho, Dominic Decherf almaarufu Papa Oyoo ndiye huwa mpatanishi wao kila mambo yanapoharibika, jambo ambalo kulingana naye ni la kawaida sana.

“Unafikiri una changamoto katika ushirikiano wa malezi? Subiri hadi asusie maagizo yalizotolewa na sheria ������ Mahakama hiyo hiyo alijipeleka mwenyewe ���������," Akothee alisema.

Aliongeza, “Namshukuru Mungu kwa baba Oyoo mpatanishi,huyu mwingine angekuwa amenizika.”