Arrow Bwoy azungumza kuhusu kutengana na Nadia Mukami

"Hakuna mtu anayeanzisha uhusiano na ndoto ya kuvunja," alisema.

Muhtasari

•Akizungumza kwenye mahojiano, baba huyo wa mtoto mmoja alisema Nadia bado ni mpenzi wake na mama wa mtoto wake.

•Arrow Bwoy anasema wakati huo, walikuwa wametofautiana kama wanandoa wengine wowote

Nadia Mukami na Arrow Bwoy
Image: HISANI

Mwimbaji Arrow Bwoy amekana kuwahi kutengana na mzazi mwenzake Nadia Mukami kama alivyodai miezi mitatu iliyopita.

Akizungumza kwenye mahojiano, baba huyo wa mtoto mmoja alisema Nadia bado ni mpenzi wake na mama wa mtoto wake.

“Sijawahi kutoa taarifa na wala sijawahi kuondoka wala kuachwa na mtu, kwanza nijuavyo mimi Nadia ni mama wa mtoto wangu na mpenzi wangu,” alisema.

"Sijawahi kusema tumeachana, na ikitokea wakati kama huo utafika, hata hatutawajulisha watu kwamba tumeachana."

Arrow Bwoy aliongeza kuwa ndoto yake ni kuona kwamba uhusiano wake na Nadia umefanikiwa.

"Hakuna mtu anayeanzisha uhusiano na ndoto ya kuvunja."

Mwezi Desemba, Nadia alisema walimaliza uhusiano wao kitambo lakini wakachagua kuficha.

Nadia alieleza kwamba hawezi kuendelea kusema uwongo kuhusu hali halisi ya uhusiano wao.

"Ili tu kuwafafanulia watu ili wabook Arrow Bwoy na mimi. Nimeishiwa na uwongo. Hatujakuwa pamoja kwa muda, tuliachana," aliandika.

Arrow Bwoy anasema wakati huo, walikuwa wametofautiana kama wanandoa wengine wowote.

“Mambo huchemka kwa uhusiano, na mnapotofautiana, mpe muda,” alisema

"Tulitofautiana lakini ni kawaida kwa uhusiano wowote, tunachukulia tofauti. Labda wakati huo aliona ni sawa kupost kutokana na shinikizo, lakini nina uhakika amejifunza. Sisi ni wanandoa wachanga na bado tunajifunza. ."