"Hana kitu!" Pritty Vishy afichua kwa nini wavulana wadogo wanamtongoza mamake kwa jumbe za mapenzi

Vishy alisema kuwa yuko tayari kumwacha mama yake achumbiane lakini na wanaume wa rika lake tu na sio vijan

Muhtasari

•Pritty Vishy alisisitiza kwamba wamekuwa wakipokea jumbe nyingi sana kutoka kwa vijana wenye umri wa ujana.

•Hata hivyo, alithibitisha kuwa mama yake hayupo kwenye mahusino na wala hachumbii na mtu yeyote kwa sasa.

Pritty Vishy na mama yake.
Image: INSTAGRAM// PRITTY VISHY

Mtayarishaji wa maudhui maarufu wa Kenya, Purity Vishenwa almaarufu Pritty Vishy ameweka wazi kwamba mama yake si tajiri wa kutosha kuwafadhili vijana wadogo ambao wameendelea kufungua roho na kukiri kumpenda.

Katika mahojiano ya simu na kituo kimoja cha redio cha humu nchini, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22 alisisitiza kwamba wamekuwa wakipokea jumbe nyingi sana kutoka kwa vijana wenye umri wa ujana wakikiri mapenzi yao kwa mama yake na kuomba kuwa mpenzi wake.

Vishy alidai kuwa vijana kama hao wanamfuata mama yake kwani wanadhani ana pesa nyingi za kuwafadhili, jambo ambalo kwa mujibu wake sivyo.

“Wanasema kwa sababu Pritty hatumuoni, labda tujaribu mama yake. Mama yangu si mgeni katika mambo haya. Anauliza tu, ‘Pury hizi ni nini?,” Pritty Vishy alisema.

Aliongeza, “Ni watoto tu wajinga wanadhani ako na pesa. Nina ujumbe kwao, mama yangu hawezi kuwa mumamaz, hana pesa za kuwasaidia. Labda wanadhania watapata mama wa rent, jamani mama yangu hana kitu. Hatuna hiyo pesa. Watafute kwingine,”

Mpenzi huyo wa zamani wa mwimbaji Stevo Simple Boy hata hivyo alithibitisha kuwa mama yake hayupo kwenye mahusino na wala hachumbii na mtu yeyote kwa sasa.

Alisema kuwa yuko tayari kumwacha mama yake achumbiane lakini na wanaume wa rika lake tu na sio vijana na wale ambao hawawezi kumtunza.

"Mama yangu alipata mimba akiwa na umri wa miaka 14. Tangu mama yangu aanze kuchumbiana, hajakuwa na bahati ya kuwa na mwanaume anayejali ambaye atamtunza na ninamtakia mema. Nadhani akileta mtu nione hawazei kumshughulikia nitamwambia kwaheri tu,” alisema.

Mtayarishaji wa maudhui huyo mwenye umri wa miaka 22 alidai kuwa wavulana hao wadogo wamekuwa wakimlenga mamake kwani waliona kwamba yeye hakuwajibu ujumbe.

Alidai kuwa kuna jumbe nyingi sana zinazotumwa kwa mamake kwenye mitandao ya kijamii na vijana ambao wamekuwa wakimmezea mate.