"Je, naweza kudai ng'ombe?" Akothee ajawa bashasha baada ya kukutana na mpenzi wa bintiye mdogo (+picha)

"Hakuna mahari iliyotajwa. Nataka tu uwe na furaha, na ninaweza kukuona una furaha," Akothee alimwambia bintiye.

Muhtasari

•Fancy Makadia aliandamana na mpenzi wake Faïrouz Vivian Ligali Ali alipokutana na mama yake na watatu hao walifurahia mlo pamoja.

•Akothee hakudai chochote kutoka kwa mpenziwe Makadia na akasema ameridhika kuona bintiye akiwa na furaha.

alijawa na bashasha baada ya kukutana na bintiye na mpenzi wake.
Akothee alijawa na bashasha baada ya kukutana na bintiye na mpenzi wake.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee alijawa na bashasha baada ya kukutana na mpenzi wa binti yake mdogo Fancy Makadia.

Fancy Makadia aliandamana na mpenzi wake Faïrouz Vivian Ligali Ali alipokutana na mama yake na watatu hao walifurahia mlo pamoja.

Katika video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Akothee alimshukuru bintiye na mpenzi wake kwa kujumuika naye kwenye mlo huo na akakiri angependa kufurahia muda nao tena.

"Katika maisha yangu yajayo nataka kuwa kama nyinyi, kuendesha gari tu kuzunguka ulimwengu. Nafikiri niko makini sana na maisha,” Akothee alisema.

Katika video iliyoshirikiwa na mama huyo wa watoto watano, watatu hao walionekana kuwa na furaha pamoja na Akothee hata alisikika akitaniana na bintiye na shemeji huyo wake.

"Je, naweza kudai ng'ombe sasa au baadaye," Akothee alimwuliza bintiye.

Makadia alimfahamisha mama yake kuwa yuko huru kudai mahari kutoka kwa mpenzi wake na kumtaka afafanue anachotaka.

Akothee hata hivyo hakudai chochote kutoka kwa mpenziwe Makadia na akasema ameridhika kuona bintiye akiwa na furaha.

"Hakuna bei iliyotajwa. Nataka tu uwe na furaha, na ninaweza kukuona una furaha. Asante kwa ajili yetu (Ali). Mtoto wangu anaonekana kutunzwa vizuri,” alisema.

Mnamo Aprili 19, 2023, Fancy Makadia alitangaza uhusiano wake hadharani.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Fancy kumtambulisha mpenzi wake duniani lakini sura ya mtu wake ilikuwa imefifia kwenye picha aliyoshiriki.

Haya wewe, nimebarikiwa sana kuwa na wewe kama sehemu ya maisha yangu. Asante kwa kuwa mpenzi wangu, rafiki yangu, na msiri wangu.

“Upendo wako umenipa ujasiri wa kuushinda ulimwengu huu. Ninakushukuru kwa kunifanya kuwa mtu bora zaidi. Ungeweza kuwa na mtu yeyote katika ulimwengu huu, lakini ulinichagua mimi. Asante.

"Nakupenda OC (Osiep Chunya)," Fancy Makadia alinukuu picha akiwa na mpenzi wake ambaye alifichwa uso.

Hatua hiyo iliwafanya wanamitandao kuchimba zaidi wakijaribu kufichua sura ya bintiye Akothee.