Kajala afunguka kuhusu Harmonize kumfumania akim'cheat na mwanaume mwingine

Kajala amemtaka Harmonize kuweka mambo wazi iwapo usaliti wa kimapenzi ndio sababu ya wao kuachana.

Muhtasari

•Kajala amemtaka Harmonize kujitokeza na kuweka mambo wazi iwapo alimsaliti kimapenzi katika kipindi cha miezi kadhaa ambayo walichumbiana mwaka jana.

•“Aje aseme kama alinifumania ama nilimcheat aseme. Kama aliweza kuandika vitu vingine aseme,” Kajala alisema.

Kajala na Harmonize wakati mahaba yao yalikuwa yamenoga
Image: HISANI

Kajala Masanja amemtaka aliyekuwa mpenzi wake Harmonize kujitokeza waziwazi na kuweka mambo wazi iwapo alimsaliti kimapenzi katika kipindi cha miezi kadhaa ambayo walichumbiana mwaka jana.

Muigizaji huyo mkongwe wa filamu bongo alitoa agizo hilo kwa Konde Boy wakati akijibu madai kuwa bosi huyo wa Konde Music Worldwide aliwahi kumfumania akimcheza na mwanaume mwingine baada ya kupitia simu yake.

Kajala amemtaka staa huyo wa bongo fleva kuweka mambo wazi iwapo usaliti wa kimapenzi ndio sababu ya wao kuachana mwishoni mwa mwaka jana.

“Aje aseme kama alinifumania ama nilimcheat aseme. Kama aliweza kuandika vitu vingine aseme,” Kajala alisema.

Wakati akizungumza na mtayarishaji Director Kenny katika video ambayo alichapisha takriban miezi mitatu iliyopita,  Harmonize alidokeza kuwa mahusiano yake yalisambaratika baada ya kupata mpenzi wake ambaye hakubainisha wazi ni nani akiwa ametumiwa meseji ya kimapenzi na mwanamume mwingine.

“Nilikuta meseji kwenye simu yake, mwanaume akiwa amemtumia meseji. Alianza kuniripukia kana kwamba anataka kupigana na mimi, nikamwambia sitaki kupigana naye, huwa sipigani na wanawake. Nilimwambia achukue simu yake," Konde Boy alimhadithia Director Kenny kwenye video iliyochapishwa YouTube.

Bosi huyo wa Kondegang alibainisha kwamba alisikitika sana kutokana na tukio hilo kiasi cha kukata tamaa na mapenzi.

Hata hivyo, baadaye aliweka wazi kuwa video hiyoilikuwa ni sanaa tu na mazungumzo yake na Kenny hayakuwa  kuhusu sababu halisi ya yeye kuachana na muigizaji Frida Kajala Masanja mwishoni mwa mwaka jana.

 "Stori iliyo ndanio haihusiani kabisa na uhalisia wa maisha yangu. Stori imetunga na kuongozwa na Director Kenny. Aliwaza nini?? Sijuwi kiukweli," alisema.

Wengi hata hivyo walichukulia mazungumzo ya Harmonize na Kenny kama dokezo ya sababu ya yeye kutengana na Kajala.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio cha humu nchini mwezi Aprili, Kajala hata hivyo alidokeza kuwa alimtema mwimbaji huyo kwa sababu ya mazoea.

"Sijui niseme nini. Labda mazoea. Mtu akishakuzoea sana anakuchukulia poa," Kajala alisema.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alidokeza kwamba Harmonize bado hakuwa tayari wakati alipoamua kutulia naye kwenye mahusiano na kuwa huenda alihitaji nafasi ya kufanya mambo yake binafsi.

"Yaani mimi hata simlaumu, kwa sababu yeye ni kijana mdogo. Labda alihitaji nafasi, tulikuwa tuko karibu sana.

Yeye mara ya kwanza nahisi labda aliona kama mzaha akisema nataka huyu mtu, nataka niwe naye 24/7.  Mnaamka wote mnaenda gym, mnafanya hiki na kile. Labda alikuwa anahitaji nafasi yake afanye vitu vyake," alisema.

Kajala alibainisha kwamba alikubali kurudaina na bosi huyo wa Konde Music Worldwide kwa kuwa bado alikuwa anampenda.