Karen Nyamu ajibu baada ya kukejeliwa kwa madai ya kufuata sehemu ya siri ya Samidoh

Nyamu alidokeza kuwa tayari ana dhahabu na kitu pekee alichobaki kutafuta ni sehemu ya siri ya mwanamume.

Muhtasari

•Shabiki alimdhihaki kwa madai ya kukimbilia sehemu ya siri ya mwimbaji Samidoh badala ya kukimbiza dhahabu kama Kipyegon.

•Nyamu alidokeza kuwa tayari ana dhahabu na kitu pekee alichobaki kutafuta ni sehemu ya siri ya mwanamume.

Samidoh na Karen Nyamu
Image: FACEBOOK// KAREN NYAMU

Jumanne usiku, seneta Karen Nyamu alimpongeza mwanariadha wa Kenya Faith Kipyegon kwa kushinda mbio za mita 1500 katika Mashindano ya Dunia yanayoendelea jijini Budapest, Hungary.

Katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook, Nyamu alimpongeza mshikilizi huyo wa rekodi ya dunia katika mbio hizo kwa kushinda dhahabu ya kwanza kwa Kenya katika mashindano hayo.

"G.O.A.T! Dhahabu ya kwanza kwa Kenya katika Mashindano ya Budapest,” Nyamu aliandika chini ya picha ya mwanariadha huyo akiwa ameshikilia bendera ya Kenya.

Kama ambavyo imekuwa kawaida, baadhi ya wanamitandao walitumia sehemu ya maoni ya chapisho la mwanasiasa huyo kumdhihaki kuhusu mahusiano yake.

Mtumiaji wa Facebook alimdhihaki kwa madai ya kukimbilia sehemu ya siri ya mwimbaji Samidoh badala ya kukimbilia dhahabu kama Kipyegon.

“Watu wanatafuta dhahabu, alafu kuna wewe unatafuta sehemu ya siri ya Thamweli (Samidoh). Ona maisha yako,” Givens Musine alitoa maoni.

Katika majibu yake, mama huyo wa watoto watatu alidokeza kuwa tayari ana dhahabu na kitu pekee alichobaki kutafuta ni sehemu ya siri ya mwanamume.

“Dhahabu yangu’ niko nayo, sehemu ya siri ya mwanaume ndio sikua nayo,” alijibu.

Kwa muda mrefu, seneta huyo wa kuteuliwa amekuwa akikejeliwa sana, suala kuu likiwa uhusiano wake na staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh. Baadhi wamekuwa wakimkashifu kwa madai ya kuvunja ndoa ya miaka mingi ya mwanamuziki huyo na kumtenganisha na Bi Edday Nderitu.

Katika mahojiano ya mwezi jana, seneta Nyamu alikanusha madai ya kuvunja ndoa ya Samidoh na ya 'kumuiba' mwimbaji huyo wa Mugithi kutoka kwa mkewe wa miaka mingi, Edday Nderitu.

“Sijawahi kumuibia mtu mume, tena huyo mwanaume, nina watoto naye na anapenda watoto. Ukitaka kugombana na kutofautiana naye, jaribu kumtenga na watoto wake, wote,” alisema.

Nyamu alidokeza kuwa mzazi mwenzake ameweza kutunza nyumba zake zote mbili, yake na ya Edday Nderitu kwa miaka mingi.

Aidha, alidokeza kwamba licha ya drama zote katika maisha yake ya mahusiano, yeye ni mwanamke mwaminifu sana na huwa anampigania tu Samidoh kwa sababu ni baba wa watoto wake.

Mwanasiasa huyo aliyezingira na drama alibainisha kwamba yeye huwa hasababishi fujo kwa sababu ya mapenzi bali kwa sababu anataka watoto wake wajisikie kuwa wanatambulika.

"Watoto wangu wanakua katika mazingira hayo, hakuna wakati nitaruhusu watoto wangu wajisikie kama watoto wadogo kuliko wengine, kwamba watoto wangu hawawezi kupostiwa na baba yao lakini wengine wanaweza kupostiwa ilhali wanamjua baba yao na wana uhusiano. Nataka kurekebisha mazingira ya watoto wangu iwezekanavyo ili wawe na wazazi wanaowapenda hadi wakati ambao haitawezekana tena, ikiwa wakati huo utafika, nitakuwa nimejaribu kila wakati hivyo sitajuta," alisema.

Nyamu alisisitiza kwamba kamwe huwa hahusiki katika vita na mkewe Samidoh, Bi Edday Nderitu au kujibizana naye hata anapochokozwa.

"Chochote unachoweza kusikia nikizungumza juu yake ni kitu kizuri," alisema.