“Kwani mimi ni viazi!” Bintiye Akothee, Rue Baby alalamika baada ya dadake mdogo kupata mpenzi

"Heh Mungu, kwani mimi ni viazi, mapenzi ni matamu ooo," Rue Baby alisema.

Muhtasari

•Fancy Makadia alipakia video iliyomuonyesha akiwa na wakati mzuri na kijana aliyetambulika kwa jina la Fairouz Vivian Ligali Ali.

•Katika jibu lake, Akothee alionekana kuidhinisha uhusiano wa bintiye na Fairouz na kuwapa mamlaka ya kufurahia.

Rue Baby na dadake Fancy Makadia
Image: INSTAGRAM// FANCY MAKADIA

Binti mdogo wa mwimbaji Akothee, Fancy Makadia, alimuonyesha mpenzi wake kwa walimwenguni siku ya Jumanne asubuhi.

Katika ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 21 alipakia video iliyomuonyesha akiwa na wakati mzuri na kijana aliyetambulika kwa jina la Fairouz Vivian Ligali Ali. Alinukuu video hiyo kwa emoji ya moyo kuashiria mapenzi.

Wapenzi hao wawili walionekana wakikumbatiana na kubusiana kwenye video hiyo.

Akothee alikuwa miongoni mwa wanamitandao wa kwanza kutoa maoni kwenye chapisho la bintiye. Katika jibu lake, mama huyo wa watoto watatu alionekana kuidhinisha uhusiano huo na kuwapa mamlaka ya kufurahia.

“Auuu haki mapenzi wewe, furahia mpendwa wangu,” Akothee alisema.

Mwingine aliyetoa maoni yake ni binti wa pili wa mwimbaji huyo, Rue Baby ambaye kimzaha alionyesha wivu kwa mahusiano ya dada yake.

"Heh Mungu mimi ni viazi, mapenzi ni matamu ooo," Rue Baby alisema.

Haya yanajiri baada ya Makadia na mpenzi huyo wake kukutana na mama yake barani  Ulaya na kufurahia mlo pamoja.

Katika video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Akothee alimshukuru bintiye na mpenzi wake Ali kwa kujumuika naye kwenye mlo huo na akakiri angependa kufurahia muda nao tena.

"Katika maisha yangu yajayo nataka kuwa kama nyinyi, kuendesha gari tu kuzunguka ulimwengu. Nafikiri niko makini sana na maisha,” Akothee alisema.

Katika video iliyoshirikiwa na mama huyo wa watoto watano, watatu hao walionekana kuwa na furaha pamoja na Akothee hata alisikika akitaniana na bintiye na shemeji huyo wake.

"Je, naweza kudai ng'ombe sasa au baadaye," Akothee alimwuliza bintiye.

Makadia alimfahamisha mama yake kuwa yuko huru kudai mahari kutoka kwa mpenzi wake na kumtaka afafanue anachotaka.

Akothee hata hivyo hakudai chochote kutoka kwa mpenziwe Makadia na akasema ameridhika kuona bintiye akiwa na furaha.

"Hakuna bei iliyotajwa. Nataka tu uwe na furaha, na ninaweza kukuona una furaha. Asante kwa ajili yetu (Ali). Mtoto wangu anaonekana kutunzwa vizuri,” alisema.

Mnamo Aprili 19, 2023, Fancy Makadia alitangaza uhusiano wake hadharani.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Fancy kumtambulisha mpenzi wake duniani lakini sura ya mtu wake ilikuwa imefifia kwenye picha aliyoshiriki.

Haya wewe, nimebarikiwa sana kuwa na wewe kama sehemu ya maisha yangu. Asante kwa kuwa mpenzi wangu, rafiki yangu, na msiri wangu.

“Upendo wako umenipa ujasiri wa kuushinda ulimwengu huu. Ninakushukuru kwa kunifanya kuwa mtu bora zaidi. Ungeweza kuwa na mtu yeyote katika ulimwengu huu, lakini ulinichagua mimi. Asante.

"Nakupenda OC (Osiep Chunya)," Fancy Makadia alinukuu picha akiwa na mpenzi wake ambaye alifichwa uso.

Hatua hiyo iliwafanya wanamitandao kuchimba zaidi wakijaribu kufichua sura ya bintiye Akothee.