Mambo imechemka! Brown Mauzo athibitisha kutengana na Vera Sidika

Alisema waliamua kuachana lakini hakutoa sababu hasa iliyopelekea uamuzi huo.

Muhtasari
  • Kulingana na yeye, wamepitia nyakati zisizosahaulika na kuenda njia tofauti ulikuwa uamuzi bora kwao na kwa watoto wao.
wamemuonyesha mtoto wao kwa mara ya kwanza
Vera Sidika na mumewe Brown Mauzo wamemuonyesha mtoto wao kwa mara ya kwanza
Image: INSTAGRAM//

Msanii wa muziki  Brown Mauzo ametangaza kutokuwa tena kwenye mahusiano na Vera Sidika ambaye ni mama wa watoto wake wawili.

Mauzo alitangaza habari hizo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii. Alisema waliamua kuachana lakini hakutoa sababu hasa iliyopelekea uamuzi huo.

Kulingana na yeye, wamepitia nyakati zisizosahaulika na akabainisha kuwa kuenda njia tofauti ulikuwa uamuzi bora kwao na kwa watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tuliamua kuachana. Safari yetu imejaa nyakati zisizoweza kusahaulika lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia na Ice kusonga mbele tofauti," baba huyo wa watoto watano alisema.

Pia aliwashukuru marafiki na wafuasi wao kwa kusimama nao kwa muda ambao wamekuwa pamoja.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na msaada katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutia moyo kwako kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wako na heshima yako kwa faragha yetu wakati huu," Brown Mauzo alisema.

"Ingawa njia zetu zinaweza kutofautiana tutathamini kumbukumbu ambazo tumeunda pamoja. Sote wawili tunasalia kushukuru kwa masomo tuliyojifunza,” aliongeza.

Habari hizi zinajiri siku chache baada ya veera kurejea nchini kutoka dubai.