Ngesh wa Vasha azungumzia madai ya kuwa mwanachama wa LGBTQ

“Mimi niko na mtu. Nadate. Ako Naivasha,” Ngesh alisema.

Muhtasari

•Katika mahojiano na, rapa huyo chipukizi alibainisha kwamba hata hajui herufi LGBTQ zinasimamia nini.

•Ngesh alifichua kuwa kwa sasa yuko kwenye mahusiano na mwanamume ambaye anaishi nyumbani kwao, Naivasha.

Ngesh wa Vasha
Image: HISANI

Mwimbaji chipukizi wa Kenya Mary Wangeci almaarufu Ngesh wa Vasha amekanusha madai kuwa yeye ni mwanachama wa LGBTQ.

Katika mahojiano na mwanahabari Vincent Mboya, rapa huyo kijana alibainisha kwamba hata hajui herufi LGBTQ zinasimamia nini.

“Mimi siwezi kuwa na nini kama hizo. Mimi ata sijui maana ya herufi hizo,” Ngesh alisema.

Mwimbaji huyo wa kibao 'Kaveve Kazoze’ pia aliweka wazi kuwa hakuna mwanamke yeyote amechukua hatua ya kumtongoza kwa nia ya kuchumbiana naye, kinyume na tetesi ambazo zimekuwa mjini. Tangu alipopata umaarufu, kumekuwa na tetesi kwamba Ngesh huenda ni msagaji kwa kuzingatia mtindo wake wa mavazi na mwonekano wake.

Katika mahojiano na Mboya, Ngesh pia alifichua kuwa kwa sasa yuko kwenye mahusiano na mwanamume ambaye anaishi nyumbani kwao, Naivasha.

“Mimi niko na mtu. Nadate. Ako Naivasha,” Ngesh alisema.

Ngesh ni mwanachama wa kundi la muziki la Spider Clan ambalo lilipata umaarufu mwezi uliopita baada ya wimbo wao wa ‘Kaveve Kazoze’ kuvuma mitandaoni.

Kundi la Spider Clan lina wanabendi wanne ambao ni; Ngesh, Banguz, Ngesh, Nguzu, na Mosray. Ngesh, Mguzu, na Mosray ni ndugu na mwezi uliopita walizungumzia vipaji vya muziki katika DNA zao.

Wao ni familia ya wanamuziki kulingana na maelezo waliyotoa kwa KTN. "Ni kitu hamjui, huyu ni siz yangu na huyu ni bro," mmoja wa ndugu alibainisha. 

Mwanachama wa mwisho, Banguz ni jirani. Walianza muziki wao baada ya Banguz kuwahimiza kuunganisha nguvu na kujitosa kabisa kwenye tasnia.

Jina la Spider Clan lilichaguliwa kuwa Banguz ambaye alisema, "Spider hurusha mawebs, sasa sisi tukaamua turishe ma vibes." Ni majirani nyumbani kwao katika eneo la Nyandarua. 

Mnamo Juni 19, Ngesh alitumbuiza kwenye tamasha lake la kwanza la klabu katika mji wa Muranga. Video za kipindi hicho ziliwafanya Wakenya wampigie debe, wakibainisha kwamba alikuwa anaelekea kupata umaarufu mkubwa. Ngesh pia ametia saini mkataba wa kurekodi.