"Nilimwambia mtoto babake aligongwa na treni!" Carrol Sonie akiri wakirushiana vijembe na Mulamwah

Sonie alikiri kum’block ex wake, kumnyima nafasi ya kumuona mtoto na kumdanganya bintiye kuwa baba yake alikufa.

Muhtasari

•Mulamwah alilalamikia ku’blockiwa na baby mama, kumuona mtoto tu mtandaoni, kuonekana kuwa tatizo, kuchukiwa na mzazi mwenzake, miongoni mwa mengine.

•"Of course I am a toxic baby mama, nilimwambia binti yangu kuwa babake aligongwa na treni akiwa kazi ya reli," Sonie alisema.

Carrol Sonnie na aliyekuwa mpenzi wake Mulamwah
Image: HISANI

Muigizaji Caroline Muthoni Ng’ethe almaarufu Carrol Sonie amejibu baada ya aliyekuwa mpenzi wake, David Oyando almaarufu Mulamwah kuonekana kumtupia vijembe katika video ya hivi majuzi ya challenge ya “Of course I am a Baby Daddy in Kenya.”

Katika video yake ya burudani, Mulamwah alisikika akiangazia baadhi ya changamoto za kuwa baby daddy, akionekana kuzungumza kuhusu hali yake na Sonie.

Miongoni mwa mambo ambayo mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alilalamikia ni ku’blockiwa na baby mama, kumuona mtoto tu mtandaoni, kuonekana kuwa tatizo, kuchukiwa na mzazi mwenzake, miongoni mwa mengine.

"Of course I am a baby daddy in Kenya, everybody thinks I am the problem.. Ofcourse I am a baby daddy in Kenya, kila baby mama ananichukia, aki tafadhali auntie sio mimi nilikupa mimba," Mulamwah alisikika akisema kwenye video hiyo.

Aliendelea, “Of course I am a baby daddy in Kenya, mtoto alishaambiwa na anajua nilikufa mwaka jana. Of course I am a baby daddy in Kenya, nikitesa wanasema naumiza ex, na mimi niko tu maisha yangu, sasa nisioe? Bila shaka mimi ni baba mtoto nchini Kenya, mtoto namuonea tu mtandaoni. Of course I am a baby daddy in Kenya, bila shaka najipanga panga kwa sababu najua kuna siku nitahitajika. Of course I am a baby daddy in Kenya, nimeblockiwa. Ofcourse I am a baby dady in Kenya, hakuna mtu ataniamini lakini ni sawa."

Kweli, ujumbe huo ulionekana kumfikia mtu aliyelengwa, Carrol Sonie ambaye alijibu pia kwa kufanya video ya "Of course I am a toxic baby mama."

Katika majibu yake, muigizaji huyo alionekana kukiri kum’block mpenzi wake huyo wa zamani, kumnyima nafasi ya kuonana na mtoto na kumdanganya mtoto kuwa baba yake alikufa.

“Of course I am a toxic baby mama, ata ex akinitext na pseudo account eti ananimiss, ata hiyo nablock. Ofcourse I am a toxic baby mama ‘Keilah is not my kid’ ataendelea kumuonea mitandaoni,” Carrol Sonie alisema kwenye video hiyo aliyoitengeneza na kuichapisha.

Aliongeza, “Of course I am a toxic baby mama, Mkikuyu kusema kweli, tutihakagwo macuru. Of course I am a toxic baby mama, nilimwambia binti yangu kuwa babake aligongwa na treni akiwa kazi ya reli. I am a toxic baby mama, mimi ndiye hupatia baby daddy content, hawezi kufanya bila mimi.

Ingawa hawakutajana majina, wapenzi hao wa zamani walionekana kushambuliana kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kurushiana tuhuma na kuangazia jinsi uhusiano wao wa sasa ulivyo.