Ruth K azungumza kuhusu alichofanya kumfanya Mulamwah apagawe juu yake

Ruth alidai kuwa siri imekuwa ni kumuweka Mulamwah vizuri k.m kwa kumpikia vizuri.

Muhtasari

•Wachekeshaji YY na Butita walionekana wakimhoji mtayarishaji wa maudhui wakitaka afichue alichomfanyia Mulamwah.

•"Mazee, ulipea boy wetu nini, hiyo ndio kitu tunajiuliza.. sisi tunashindwa bana, kuna vitu anafanya ata sisi tunashindwa bana," walisema.

Mulamwah na mpenzi wake Ruth K.
Image: INSTAGRAM// RUTH K

Waigizaji wa vichekesho Eddie Butita na YY walimtania mpenzi wa Mulamwah, Ruth K wakimtaka atoe siri ya kile alichompa ili kumfanya ampende sana jinsi anavyompenda.

Katika video fupi ambayo YY alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, wachekeshaji hao wawili walionekana wakimhoji mtayarishaji wa maudhui wakitaka afichue alichomfanyia Mulamwah.

“Mazee, ulipea kijana wetu nini.. ulimpeanga nini?,” YY na Butita waliuliza kwa pamoja.

Wawili hao waliendelea kumsifu Ruth K wakidai kuwa mchekeshaji huyo mwenzao amekuwa aking’ara zaidi na amekuwa na furaha zaidi tangu waanze kuchumbiana.

“Huyu boy ni wewe anaongelea tu saa zote, yaani saa zote ni stori zako tu anapiga. Huyu boy ata ikifika saa kumi na moja anasema nataka kwenda kuona Ruth, nataka kwenda kuona bestie acha nifike kwa nyumba na nini,” YY alisema.

Ruth akajibu, “Anapea bestie wakati. Kwa nyumba ya 6, hakuna kuchelewa.”

YY na Butita waliendelea kumshinikiza mtayarishaji maudhui huyo ambaye kwa sasa ana ujauzito wa mtoto wake wa kwanza wa Mulamwah afichue alichomfanyia mchekeshaji huyo.

"Mazee, ulipea boy wetu nini, hiyo ndio kitu tunajiuliza.. sisi tunashindwa bana, kuna vitu anafanya ata sisi tunashindwa bana," walisema kwa pamoja.

Ruth ambaye kwa kawaida huwa anamtambua Mulamwah kama ‘bestie’ alidai kuwa siri imekuwa ni kumweka Mulamwah vizuri k.m kwa kumpikia vizuri.

Baada ya Ruth kuondoka katika eneo la mazungumzo hata hivyo, ilionekana wazi kuwa YY na Butita walikuwa wakimtania tu ili kumfanya ajisikie furaha, anayependwa na kuthaminiwa. Walionekana wakimuuliza Mulamah kama walikuwa wamepiga shoo nzuri mbele ya mpenzi wake, ishara kuwa yote ilikuwa utani.

Kufikia mwisho wa mwezi Novemba, Mulamwah na Ruth hatimaye walifichua kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja baada ya kukana kwa muda mrefu. Kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii, wawili hao walionyesha picha zao zikionyesha tumbo la Ruth lililochomoza, wakidokeza kwamba hayuko mbali na kujifungua.