“Samidoh ni mtu wa kunyima surely!” Karen Nyamu ajibu madai ya uasherati

Seneta Nyamu alionekana kusisitiza uaminifu wake kwa mpenzi wake Samidoh.

Muhtasari

•Shabiki alitoa maoni katika kile kilichoonekana kama onyo lililoashiria kwamba seneta huyo wa UDA anajiingiza katika zinaa.

•Nyamu alidokeza kuwa licha ya drama zote katika maisha yake, yeye ni mwanamke mwaminifu sana na huwa anampigania tu Samidoh kwa sababu ni baba wa watoto wake.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Wakili mashuhuri na ambaye ni seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu amejibu kwa utani baada ya kukabiliwa na tuhuma za uasherati.

Mama huyo wa watoto watatu alikuwa amechapisha kwenye mtandao wa Facebook wakati mwanamitandao alipotoa maoni huku akionyesha upendo wake mkubwa kwake.

“Napenda tu moyo wako, imagine huyu mhesh ni roho safi ukimsikiza vizuri,” mtumizi wa Facebook alisema chini ya chapisho la Karen Nyamu.

Chini ya maoni hayo, mtumizi mwingine wa Facebook alitoa maoni yake katika kile kilichoonekana kama onyo lililoashiria kwamba seneta huyo wa UDA anajiingiza katika zinaa.

"Anapeana kupeana hama," mwanamitandao huyo aliandika.

Kauli hiyo bila shaka ilimfikia mwanasiasa huyo mtata ambaye alionekana kuicheka tu, lakini wakati huo huo akachukua fursa kusisitiza uaminifu wake kwa mpenzi wake, mwanamuziki Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.

Karen aliandika, "Samidoh ni mtu wa kunyima surely."

Image: FACEBOOK// KAREN NYAMU

Katika mahojiano ya mwezi jana, Nyamu alidokeza kuwa licha ya drama zote katika maisha yake ya mahusiano, yeye ni mwanamke mwaminifu sana na huwa anampigania tu Samidoh kwa sababu ni baba wa watoto wake.

Mwanasiasa huyo aliyezingira na drama alibainisha kwamba yeye huwa hasababishi fujo kwa sababu ya mapenzi bali kwa sababu anataka watoto wake wajisikie kuwa wanatambulika na kukubalika na wazazi wote wawili..

"Watoto wangu wanakua katika mazingira hayo, hakuna wakati nitaruhusu watoto wangu wajisikie kama watoto wadogo kuliko wengine, kwamba watoto wangu hawawezi kupostiwa na baba yao lakini wengine wanaweza kupostiwa ilhali wanamjua baba yao na wana uhusiano. Nataka kurekebisha mazingira ya watoto wangu iwezekanavyo ili wawe na wazazi wanaowapenda hadi wakati ambao haitawezekana tena, ikiwa wakati huo utafika, nitakuwa nimejaribu kila wakati hivyo sitajuta," alisema.

Karen Nyamu pia alikanusha madai ya kuvunja ndoa ya Samidoh na ya 'kumuiba' mwimbaji huyo wa Mugithi kutoka kwa mkewe wa miaka mingi, Edday Nderitu.

“Sijawahi kumuibia mtu mume, tena huyo mwanaume, nina watoto naye na anapenda watoto. Ukitaka kugombana na kutofautiana naye, jaribu kumtenga na watoto wake, wote,” alisema.

Seneta huyo alidokeza kuwa mzazi mwenzake ameweza kutunza nyumba zake zote mbili, yake na ya Edday Nderitu kwa miaka mingi.