"Sio mwaka ninaoupenda tena!" Otile Brown ahuzunika moyoni baada ya kumpoteza mtoto wake

Mwimbaji Otile Brown ametangaza kifo cha ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza.

Muhtasari

•Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alifichua kwamba ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza hakufanikiwa.

•Katika taarifa yake wiki mbili zilizopita, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 30 aliapa angempa mtoto wake upendo wake wote.

Image: INSTAGRAM// OTILE BROWN

Mwimbaji wa Kenya Jacob Obunga almaarufu Otile Brown ametangaza kifo cha mtoto wake ambaye bado hakuwa amezaliwa.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili jioni, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alifichua kwamba ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza hakufanikiwa.

"Mtoto wetu hakufanikiwa.. Nadhani sio mwaka wangu pendwa tena," Otile Brown alisema kwenye mtandao wa Instagram.

Aliongeza, "Yote ni nzuri. Mungu unajua sijawahi kukuuliza wala kukuhoji.. ninachofanya ni kutabasamu na kuwa sawa.

Baada ya kutangaza habari hizo za kusikitisha, mwanamuziki huyo aliendelea kufuta picha zote kwenye akaunti yake ya Instagram, jambo linaloashiria kuwa mambo si sawa.

Haya yanajiri takriban wiki moja tu baada ya mwanamuziki huyo mzaliwa wa Pwani kutangaza anatarajia mtoto wake wa kwanza.

Katika taarifa yake wiki mbili zilizopita, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 30 aliapa angempa mtoto wake upendo wake wote.

"Bizeee hivi karibuni atakuwa papa, Inshallah.. Nitakupenda sana mtoto #Inshaallah," Otile Brown alisema kupitia mtandao wa Instagram.

Mwanamuziki huyo mahiri hata hivyo hakufichua maelezo ya mwanamke ambaye angekuwa mzazi mwenzake au jinsia ya mtoto aliyetarajia.

Tangu kutangaza utengano wake na mrembo wa Ethiopia, Nabayet mapema mwaka jana, Otile Brown amekuwa msiri  sana kuhusu mahusiano yake.

Mwimbaji huyo alichumbiana na Nabayet kwa takriban miaka minne kabla ya kutangaza kutengana kwao mwaka jana. Kabla ya kujitosa kwenye mahusiano na mrembo huyo wa Ethiopia alichumbiana na Vera Sidika.

Wakati akichumbiana na Vera Sidika miaka  kadhaa iliyopita, Otile Brown alidaiwa kumtunga mimba mwanasosholaiti huyo .

Mama huyo wa watoto wawili hata hivyo alidaiwa kutoa ujauzito huo, madai ambayo mara nyingi ameyatupilia mbali.