Vera Sidika afunguka kuhusu mpenzi wake mpya kuwa shoga

Mwanasosholaiti Vera Sidika amelazimika kujibu madai kwamba mwanamitindo huyo wa Jamaica ni shoga.

Muhtasari

•Vera amebainisha kuwa sio wanamitindo wote wa kiume ni mashoga na kuwaonya watu dhidi ya kukimbilia kwenye hitimisho.

•Hii ilifuatia madai mengi yaliyoibuliwa na wanamitandao ambao walikumbana na picha na video zenye utata za Brown.

amemtambulisha Gideon Brown kama mpenziwe mpya.
Vera Sidika amemtambulisha Gideon Brown kama mpenziwe mpya.
Image: INSTAGRAM//

Saa chache tu baada ya kufichua mpenzi wake wa sasa, Gideon Brown, mwanasholaiti wa Kenya Vera Sidika amelazimika kujibu madai kwamba mwanamitindo na mwanadensi huyo wa Jamaica ni shoga.

Vera alifichua utambulisho na akaunti ya Instagram ya mpenzi wake mnamo Jumatano jioni na Wakenya waliokuwa na shauku walipiga hatua ya kupitia ukurasa wa mwanamitindo huyo na kuibua madai kwamba huenda ni shoga.

Wakati akijibu tuhuma zilizotolewa dhidi ya mridhi huyo wa Brown Mauzo, mwanasosholaiti huyo alisema kuwa sio wanamitindo wote wa kiume ni mashoga na kuwaonya watu dhidi ya kukimbilia kwenye hitimisho.

"Nyinyi nyote mnaelewa kuwa sio wanamitindo wote wa kiume ambao ni LGBTQ, sawa? Kwa nini watu wanakimbilia kwenye hitimisho inanishangza?" Vera Sidika alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kauli ya mwanasosholaiti huyo ilifuatia madai mengi yaliyoibuliwa na wanamitandao wa Kenya ambao walikumbana na picha na video zenye utata za Bw Brown.

Vera alimtambulisha mwanamitindo huyo wa Jamaika kama mpenzi wake mpya mpya kwa mashabiki wake mtandaoni siku ya Jumatano jioni alipochapisha picha yake na kuiambatanisha na ujumbe wake ukimuhakikishia kwamba anampenda sana.

“Nakupenda milele baby!! @itsgbrown,” Vera aliandika.

Brown alichapisha tena posti ya mwanasososholaiti huyo wa Kenya na pia kukiri kumpenda, "Nakupenda mpenzi."

Haya yanajiri takriban mwezi mmoja na nusu tu baada ya mwimbaji Brown Mauzo kutangaza kuachana na mama huyo wa watoto wake wawili.

Mwishoni mwa mwezi Agosti, Mauzo alitangaza kuwa yeye na Vera wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Alishukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"

Aidha, alidokeza kuwa ukurasa  unaofuata wa maisha yao utakuwa kuhusu uponyaji wa moyo baada ya kuachana na kukumbatia yake yaliyo mbele.