Hisia zatanda huku Bensoul akitangaza kifo cha mamake wakati akitumbuiza jukwaani (+video)

"Pumzika kwa amani mamangu. Alituacha wiki iliyopita, lakini hapa tunapata wakati mzuri wa kumsherehekea," Bensoul alitangaza.

Muhtasari

•Mwimbaji huyo aliwafahamisha mashabiki wake kwamba alikuwa akisherehekea maisha ya mzazi huyo wake.

•Bensoul alisema katika mahojiano ya awali kwamba angeweza kusema nyimbo zake ni kali ikiwa mamake alimwambia

BenSoul katika picha ya maktaba
Image: Moses Mwangi

Benson Mutua Muia, almaarufu Bensoul alipokuwa anawatumbuiza mashabiki wake kwenye tamasha ya wiki jana aliwafahamisha kuwa mama yake Suzana amefariki.

Mwimbaji huyo aliwafahamisha mashabiki wake kwamba alikuwa akisherehekea maisha ya mzazi huyo wake  katika video ambayo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

"Pumzika kwa amani mama yangu. Alituacha wiki iliyopita, lakini hapa tunapata wakati mzuri wa kumsherehekea," aliwaambia mashabiki wake katikati ya shoo yake.

Aliongeza;

"Anaitwa Suzana, kwa hiyo mnaimba Suzana kwa upendo au sio?"

Bensoul alisema katika mahojiano ya awali na The Trend kwamba angeweza kusema nyimbo zake ni kali ikiwa mama yake alimwambia

"Sijawahi kuzungumza naye juu ya nyimbo zangu au kumtumia link, ikiwa atagundua kuwa nina wimbo mpya na wa kushangaza, ndivyo ninavyojua kuwa huo ulikuwa wimbo mzuri"

Kwenye kipindi cha uhalisia cha  "Sol Family" kwenye Sol Generations, Mama Bensoul alizungumza hadharani kwa mara ya kwanza. Alifichua maambukizi ya kifua kikuu cha Bensoul wakati mmoja.

"Sikuona mwili, niliona mifupa tu. Nilipatwa na wazimu na nilienda kutafuta madaktari na wakati huo walikuwa wamegoma," alisema.

Bensoul alikuwa ametoa historia ya aliyopitia katika kipindi cha maambukizi yake.

Tuliandika wimbo 'El Shaddai' tukiwa Rongai. Hii ni baada ya kukohoa kwa takriban mwezi mmoja na nikajiuliza tatizo ni nini.," alisema.

"Nilienda kupima Ukimwi kwa sababu nilihisi kama nilikuwa na dalili zote. Wakati mwingine unahisi kama maisha yanaisha lakini nilipima sina.

"Waligundua kuwa ni TB na kila siku, unakula chakula cha watu kama wawili."

Roho yake ipumzike kwa amani.