Majimaji kuingia studioni na wasanii wa kundi la Ethic Entertainment.

Muhtasari

• Msanii na mtangazaji almaarufu Majimaji ametangaza kuwa anakwenda kuachia kibao kipya na kundi la Ethic Entertainment.

• Majimaji aliachia picha yake pamoja na wasanii wa kundi hilo wakinywa staftahi huku akiandika kwamba kuna ngoma ambayo wanaandaa na mashabiki wataifurahia hivi karibuni.

Majimaji
Majimaji
Image: Instagram KWA HISANI

Msanii na mtangazaji almaarufu Majimaji ametangaza kuwa anakwenda kuachia kibao kipya na kundi la Ethic Entertainment.

Majimaji aliachia picha yake pamoja na wasanii wa kundi hilo wakinywa staftahi huku akiandika kwamba kuna ngoma ambayo wanaandaa na mashabiki wataifurahia hivi karibuni.

Staa huyo ambaye hajatoa muziki kwa muda mrefu baada ya ngoma yake iliyofanya vizuri #unbwogableambayo alimshirikisha kakake wa damu, Gidi.

Ifahamike kwamba mitindo ya uimbaji ya wawili hawa ni tofauti na hivyo basi mashabiki wanasubiri kuona watatumia mbinu gani kuhakikisha wanatoa ngoma ya kufurahisha macho na masikio.

Ethic Entertainment ni moja kati ya makundi ya muziki wa gengetone ambao wanazidi kufanya vizuri na hivyo basi tuntegemea kuona kazi iliyokwenda skuli watakapoingia studioni.