Redsan atema moto kwa wasanii kwenye ngoma mpya

Muhtasari

• Mkali wa muziki wa ’Dancehall’ msanii Redsan hatimaye amerejea kwenye gemu na ngoma mpya #UkiCatchWeCatch baada ya kwenda kimya kwa muda mrefu.

• Vilevile amewazungumzia wakatili ambao wanazuia muziki wake na kuwaaambia kwamba hamwezi kwa kuwa yeye ni mfalme na atazidi kuchapa kazi bila presha yoyote ile.

Redsan
Redsan
Image: Instagram KWA HISANI

Mkali wa muziki wa ’Dancehall’ msanii Redsan hatimaye amerejea kwenye gemu na ngoma mpya #UkiCatchWeCatch baada ya kwenda kimya kwa muda mrefu.

Redsan, kwenye ngoma hiyo ameonekana kuwazungumzia baadhi ya wasanii na washikadau mbalimbali wa burudani akiwaambia kwamba alikuwa miongoni mwa waanzalishi wa burudani la Kenya na anahitaji kupewa heshima yake.

Mwanamuziki huyo aidha aliongezea kwamba vyombo vya habari vimefanya mazoea kucheza ngoma za mataifa mengine huku wakidinda kucheza miziki ya wasanii wa humu nchini, jambo ambalo anasema limeua muziki wa Kenya.

“Hatuchezi na matapeli, industry sisi ndio tumejenga mimi ndio beast wa mabazenga,”aliimba Redsan.

Ifahamike kwamba Redsan alikwenda kimya kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kutoa ngoma, huku mashabiki wakijiuliza maswali mengi kuhusu hali yake na lini angerejea katika hali yake ya kuachia ngoma.

Vilevile amewazungumzia wakatili ambao wanazuia muziki wake na kuwaaambia kwamba hamwezi kwa kuwa yeye ni mfalme na atazidi kuchapa kazi bila presha yoyote ile.

Kwa sasa inasubiriwa kuona kwamba ngoma hiyo itapokelewa vipi na mashabiki na je wasanii wenzake wataichukulia vipi.