"Kina dada, jipende na maumbile yako, kataa makalio feki!" Suzanna Owiyo ashauri

Muhtasari

Suzanna Owiyo - Kina dada, jifunze kukubali maumbile yenu, ndicho kitu cha umuhimu mkubwa ambacho uko nacho.

Suzanna Owiyo
Suzanna Owiyo
Image: Instagram

Mwanamuziki mkongwe nchini Kenya Suzanna Owiyo ambaye pia ni balozi wa nia njema wa shirika la umoja wa mataifa la utunzi wa mazingira UNEP, amewahimiza wanadada Wakenya kupenda miili yao jinsi ilivyo.

Kupitia Instagram yake, Owiyo alisema wanadada wengi wamekuwa wakifurika kwenye mitandao yake wakitaka awaeleze siri ya kudumu bila kuzeeka na kutoa makunyanzi kama wengine wenye umri wake.

Alisema mpaka ile siku wanadada wa Kenya watajikubali ndio siku ataamua kuwapa siri yake ila akadokeza kwamba siri yenyewe ni kujikubali na maumbile ya mwili wako pasi na kutetereshwa na nia ya kutafuta sajari za kubadilisha muonekano halisia.

“Wanadada wadogo wananiuliza kwamba mimi nimekataa kuzeeka. Nitawajibu hili wakati mtaanza kujikubali na muonekano wa maumbile yenu. Lakini, nini nini hii kuhusu makalio bandia? Mnasondeka vitu kujichoresho maumbo tofauti katika sehemu za makali na mapaja…. Achene kujipatia msongo wa mawazo usiofaa. Kina dada, jifunze kukubali maumbile yenu, ndicho kitu cha umuhimu mkubwa ambacho uko nacho. Niite mhafidhina na mtu wa kitambo lakini makalio bandia kwangu ni HAPANA!” aliandika Owiyo.