Diana B: Nina furaha kusubiria mtoto wangu, ila sidhani kama niko tayari kwa mchakato wa kuzaa

Mwanamuziki huyo alisema anaogopa kupitia mchakato wa kuzaa kwa mara ya tatu tena, licha ya kuwa na hamu ya kumuona mwanawe wa 3.

Muhtasari

• “Miezi michache imesalia, nina furaha na hofu kwa wakati mmoja" - Diana Bahati.

Msanii na mkuza maudhui Diana Marua akionekana mwenye mawazo
Msanii na mkuza maudhui Diana Marua akionekana mwenye mawazo
Image: DianaMarua//Instagram

Kila mtu ambaye ni mpenzi wa mitandao ya kijamii kufikia sasa anajua mwanamuziki na mkuza maudhui Diana B ni mjamzito na anatarajia kujifungua mtoto wa tatu hivi karibuni.

Licha ya kudokeza kwamba anafurahia kusubiria mtoto wake na hata kupakia video na picha kadhaa mitandaoni akijiremba na kujidekeza kwa baraka hiyo ya uzao wa tatu wat umbo lake, Diana Marua pia ana woga wa kuenda kujifungua tena.

Aliweka hii wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alipakia video akitembea na kina dada wawili kuelekea chumba cha kujifungua kina mama ambapo alisema kwamab kila mara akitazama video ile inamkumbusha uchungu wa kuzaa na anaogopa kufuata mkondo ule tena licha ya kuwa na furaha ya kungoja mwanawe wa tatu.

“Mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu niliwachukua dada zangu wawili @mitch.ngoje na @glamby_varl kupata watoto katika kituo cha huduma ya afya cha @komarockmodern bila kujua kuwa mimi ndiye nitakayefuata kutoka hapo, Mungu huyu ooh. Ninaendelea kutazama video kama hizi na zinaendelea kunipa wasiwasi na baridi. Siwezi kusubiri kukutana na mtoto wangu lakini sijui kama niko tayari kupitia mchakato huu tena,” Diana Marua alidhihirisha wasiwasi wake mkubwa.

Mkuza maudhui huyo alisema kwamba ako katika hali ya vuguvugu asijue kama ana furaha au ana woga kutokana na hali hiyo, na katika video ya Jumatano ambapo wamepakia kweney ukurasa wake wa YouTube, Diana anaonekana akimuuliza mumewe kwamba sharti mmoja wao achukue mbinu mbadala ya kupanga uzazi, huku akionekana kumwambia Bahati kuchukua hatua ya kukatwa mishipa ya uume kwa sababu haiwezekani yeye kila mara ndiye anabeba mimba na maumivu yote.

Diana alisema licha ya yote bado yeye anaamini Mungu yupo na mchakato mzima utakwisha, na kuashiria kwamba huyu huenda akawa mtoto wake wa mwisho kuzaa kutokana na woga alio nao katika mchakato mzima wa kliniki.

“Miezi michache imesalia, nina furaha na hofu kwa wakati mmoja.... Chuchu zinawasha, usiku usiolalika, zahanati kutembelewa, mchakato wa kukereketa.... Weeeeeeuhhh, Lakini Mungu yuko. Ngoja nisubiri zamu yangu,” alisema Diana Marua.