Zari: Mimi sifanyi biashara ya 'forex' mitandaoni, hao ni matapeli wanatumia jina langu (+video)

Zari aliteta kwamba watu wamekuwa wakitapeliwa kwa jina lake na mwisho wa siku wanaanza kumsumbua kutaka awarudishie pesa ambazo hahusiki kutapeli.

Muhtasari

• Ni balozi wa makampuni mengi sasa, nafanya vipindi vya uhalisia runingani, lakini si biashara ya kubadilisha pesa - Zari.

Mfanyibiashara Zari Hassan amelainisha mambo kuhusu watu wanaotumia jina lake mitandaoni kuwaibia mashabiki wake wasiojua.

Zari alisema kuwa suala hilo limemchosha na imefikia wakati sasa aweke mambo wazi kuwa yeye hajihusishi hata kidogo na masuala ya biashara za mitandaoni na zile za kubadilishana sarafu.

Amewatahadharisha mashabiki wake kukoma kulaghaiwa kisha baadae kuanza kumtafuta kwa njia ya barua pepe kutaka awarudishie pesa ambazo mwanzo si yeey aliwatapeli.

Mama huyo wa watoto watano aidha pia aliongeza kwa kusema yeye hajihusishi na biashara zozote na kwamba sekta anayojikita ni ya kutangaza vyuo anuwai nchini Afrika Kusini pamoja pia na kufanya vipindi vya uhalisia runingani.

“Mwanzo kabisa mimi sifanyi biashara mitandaoni, mimi sijui kitu chochote kuhusu kubadilishana sarafu mitandaoni, sijui faida na hasara zake. Mimi nimejikita katika elimu na kufunza watu kimaarifa. Nina vyuo vingi kote Afrika Kusini. Ni balozi wa makampuni mengi sasa, nafanya vipindi vya uhalisia runingani, lakini si biashara ya kubadilisha pesa,” Zari alizungumza kwenye video aliyoipakia Instagram yake.

Mama huyo alizidi kuelezea kwamab kitu chochote unachokiona sokoni kikiuzwa kupitia kwa jina lake huyo si yeye na kuwataka mashabiki wake kuwa macho wasije wakatapeliwa na watu wanaotumia jina lake.