Wakinipenda wawili imetosha! - Haji Manara, aliyekuwa msemaji wa Yanga

Ila alitania kwamba wa tatu atakuja tu pengine ikitokea lakini si lazima.

Muhtasari

• Manara baada ya kuoa mke wa pili, alimnunulia mke wake wa kwanza gari dogo la binafsi ambapo alitetea hatua hiyo kwa kile alichokiita kama kitoka unyumba.

Haji Manara na wake zake wawili
Haji Manara na wake zake wawili
Image: Instagram

Aliyekuwa msemaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga kutoka Tanzania, Haji Manara amezungumza kuhusu familia yake na kuwa na wake wawili.

Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram alipakia picha akiwa katikati ya wanawake watatu, wawili wakiwa ni wake zake na kutania kuwa anaonekana vizuri akiwa kati ya wanawake watatu.

Hata hivyo alisema kuwa ameridhika na wawili ambao tayari anao na japo hakufutilia mbali uwezekano wa kuoa mke wa tatu, msemaji huyo alisema kuwa ikitokea nafasi pengine atajaribu bahati katika ndoa ya tatu.

Ukijiendekeza Wawili nao hawatoshi ujue. Cheki Tatu zilivyojitosheleza. Utani bhana, Wawili wanatosha, Watatu wa kazi gani? Labda itokee tu,” Manara alisema kwa utani.

Msemaji huyo wa zamani aliyepigwa marufuku ya kutojihusisha na masuala yoyote ya spoti nchini Tanzania na shirikisho la mpira TFF alioa mke wa pili mwezi mmoja uliopita.

Aliwafurahisha wengi alipofanikiwa katika juhudi zake za kuwaleta pamoja wake zake wote huku akiwanunulia zawadi mfanano.

Manara baada ya kuoa mke wa pili, alimnunulia mke wake wa kwanza gari dogo la binafsi ambapo alitetea hatua hiyo kwa kile alichokiita kama kitoka unyumba.

“Samahani sana mke wangu Ruby🙏🏻❣️ Kwa Mila na Desturi zetu Mashomvi wa Pwani , hususan Pwani ya huku kwetu Mashariki mwa bahari ya Hindi, hutuwajibisha kutoa kitoka Unyumba Kwa Mkeo,pindi umuoleapo Mke mwingine,” alisema Manara.