Muigizaji Abel Mutua akiri kutumia vibaya pesa alizopata Tahidi High

"Tumecheza na fedha kwa muongo mmoja, hatuwezi kusema uwongo kuhusu hilo," alisema.

Muhtasari

•Abel alisema yeye na mkewe walipata pesa lakini hawakuweza kueleza kile walichokifanya na mamilioni yao.

•Abel alisema alitumia pesa nyingi kusaidia marafiki.

Muongozaji wa filamu humu nchini Abel Mutua
Muongozaji wa filamu humu nchini Abel Mutua
Image: Instagram//Abel Mutua

Mcheza filamu Abel Mutua na mkewe Judy Nyawira walitumia pesa zao vibaya hadi miaka miwili iliyopita, walipofanikiwa kuwajibikia fedha zao.

Katika kipindi cha Maswali na Majibu cha hivi majuzi kwenye Joy Ride Podcast, Abel alisema yeye na mkewe walipata pesa lakini hawakuweza kueleza kile walichokifanya na mamilioni yao.

Abel alianza kufanya kazi katika kipindi cha Tahidi High kwenye runinga ya Citizen bado akiwa chuoni.

"Tumecheza na fedha kwa muongo mmoja, hatuwezi kusema uwongo kuhusu hilo," alisema.

"Tulipata ujuzi wa kifedha mwaka wa 2020. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza nilipofanikiwa kuweka mshahara wangu wa kwanza. Jambo baya zaidi ni kwamba siwezi kukaa hapa na kusema uwongo kwamba hatukuwahi kupata pesa, tulipata pesa."

Abel alisema alitumia pesa nyingi kusaidia marafiki.

"Tatizo moja ambalo tulikuwa nalo ni tabia ya kusaidia ambapo unahisi kama unataka kuokoa kila mtu. Unapata kama Sh 200k na chini ya wiki tatu, imeisha."

Muigizaji huyo alisema yeye na mkewe walifanya kozi fupi, ambayo iliwasaidia kufuatilia pesa zao.

Wakati wa mahojiano, Abel pia alizungumza juu ya shida na kumbukumbu yake, ambapo huwa anasahau mambo haraka sana.

Alitoa mfano wa wakati aliacha gari lake likinguruma na wakati alitoa pesa na kuziacha kwenye ATM.

Alipokumbuka alirudi na kukuta tayari pesa zimeenda.