Willis Raburu apunguza 30Kgs ndani ya miezi 3 tangu kufanya sajari

Wakati niliamua kufanya sajari ya Bariatric, nilikuwa na woga mwingi lakini ilinibidi kufanya - Raburu.

Muhtasari

• Uwekezaji wa maana zaidi ambao unaweza wekeza ni kwako wewe mwenyewe - Raburu.

Raburu ajipongeza kwa kufanya sajari
Raburu ajipongeza kwa kufanya sajari
Image: Instagram

Mwanahabari wa runinga ya Citizen Willis Raburu amefichua kwamba amepoteza kilo 30 za mwili wake, miezi miwili tu tangu alipoweka wazi kuwa aemfanyiwa upasuaji wa kuondoa ufuta mwilini ili kupunguza uzito.

Raburu alipakia reel kwenye Facebook yake akionesha jinsi umbile la mwili wake limebadilika na na kusema kwamba uwekezaji mzuri alioufanya ni kwa mwili wake ili kupunguza uzito ambao ulikuwa tayari umemfanya kuonekana bonge.

“Uwekezaji wa maana zaidi ambao unaweza wekeza ni kwako wewe mwenyewe. Wakati niliamua kufanya sajari ya Bariatric, nilikuwa na woga mwingi lakini ilinibidi kufanya hivyo. Nitaelezea hadithi yangu hivi karibuni lakini mpaka sasa tayari kilo 30 zimeenda hivyo. Safari bado inaendelea,” Raburu aliandika.

Mwanahabari huyo alitumia KSh 900,000 kwa upasuaji huo; wakati huo, alikuwa na uzito wa 164kg. Alikuwa amefichua kwamba ukosoaji mtandaoni na kuwa na shinikizo la damu kulichangia yeye kuamua kwenda njia ya upasuaji kufanya jitihada katika safari yake ya kupunguza uzito.

“Wakati naenda kwa upasuaji, sikuwa naendelea vizuri. Nilihitaji kwa sababu pia shinikizo langu lilikuwa juu, cholesterol yangu pia ilikuwa juu na lilikuwa suala la kuhitaji kutunza afya yangu”

Mtangazaji huyo maarufu kwa kipindi cha 10Over10 alijipata katika majibizano makali na baadhi ya wanamitandao kipindi mwili wake ulikuwa mnene na kusimangwa sana, jambo ambalo alisema ndilo lilimpa msukumo wa kuendea sajari hiyo kwani yeye na kushiriki gym ili kupunguza uzito wa mwili aliona kabisa hangeweza.