'Maisha yako ndio hadithi yako,'Lilian Ng'ang'a asema huku akizindua kitabu chake

Pia aliwashauri wasihitimisha kuwa hawana hadithi ya simulia maishani mwao.

Muhtasari
  • Juliani na Lilian wamebarikiwa na mtoto mmoja hii ni baada ya Lilian kuachana na aliyekuwa gavana wa Machakos Alfred Mutua
Image: INSTAGRAM// LILIAN NG'ANG'A

Mpenzi wake Juliani,Lilian Ng'ang'a kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ametangaza kwamba amezindua kitabu chakee.

Kulingana na Lilian kitabu hicho kinafahamika kama 'Madam First Lady'.

Juliani na Lilian wamebarikiwa na mtoto mmoja hii ni baada ya Lilian kuachana na aliyekuwa gavana wa Machakos Alfred Mutua.

Huku akitambulisha kitambu chake aliwahimiza mashabiki wake kuwa wanapaswa kufahamu kuwa maisha yao ndio hadithi yao.

Pia aliwashauri wasihitimisha kuwa hawana hadithi ya simulia maishani mwao.

"Ilikuwa furaha mwezi uliopita kuwa sehemu ya "Nairobi African Book Talk Series" ya Columbia Global Centre inayojadili #Madamfirstladymemoir.

Ni hakika. Mimi ni Mwandishi.Usihitimishe kamwe kwamba huna hadithi ya kusimulia. Maisha yako ni hadithi yako,isimuliekwa sauti kubwa,"Aliandika Lilian.