Mapenzi yanauma: Harmonize arudi kwenye kulialia kwake baada ya kuachwa na Kajala

Mitihani na majaribu kaumbiwa mwanadamu, - Harmonize alilia.

Muhtasari

• Msanii  huyo aliachia aya moja yenye kuzungumza ya moyoni kupitia Instagram yake.

harmonize akionekana mwingi wa mawazo baada ya penzi lake na Kajala kuvunjika.
harmonize akionekana mwingi wa mawazo baada ya penzi lake na Kajala kuvunjika.
Image: Instagram

Nyota wa Bongo Fleva Harmonize amerudi kwa kulia lia kwake baada ya kuachwa na mwigizaji mkongwe Kajala Masanja aliyekuwa mchumba wake.

Siku moja tu baada ya taarifa kusagaa kuwa ameachwa, Harmonize ameachia dude la kusimulia maisha yake kwa jina ‘Mwenyewe’ ambapo anaelezea jinsi alivyokuwa mpaka kufikia umaarufu wake baada ya kutusua kwenye muziki wa Bongo.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aliachia maelezo marefu ya kutoa himiza kwa wanyonge akiwashauri kutokata tamaa ya maisha kwani ni kupambana jino na ukucha na kusema kuwa wimbo huo ni kwa ajili ya watu kama hao ambapo wanapambana kutwa kucha ilmradi wapate utaalam wa kinywani kuelekea tumboni.

Kwa niaba Ya Wanangu Mtaani Na Yeyote Kutoka Familia Duni Kama mimi Amini Kwamba Hata Mshindi Wa Leo Ndio Yule Aliye Shindwa Siku Zingine Nikusisitize Tuu Kutokata Tamaa Kila siku Iwe Siku Nyengine Usilisahau Jina la MUNGU Katika kila Ulitendalo MITIHANI & MAJARIBU Kaumbiwa Mwanadamu Usikate Tamaa 💪Wimbo Huu Ukakuongezee Nguvu Katika Mihangaiko Yako,” Harmonize aliandika.

Msanii huyo alimvisha Kajala pete ya uchumba mwezi Juni mwaka huu na wengi walikuwa wanasubiria matarumbeta ya harusi lakini hali ni kama imeenda mvange kama kile ambacho tunakiona mitandaoni ni kweli.

Mpaka sasa Harmonize hajazungumza hadharani ni nini kilitokea wala kudhibitisha kuachana kwao lakini mwenzake Kajala tayari ameshamwaga ubuyu huku akisema kuwa anajuta kilichotokea ila amesamehe na sasa amejiweka tayari kwa chochote kitu ambacho maisha yatamletea.