Lukamba: Mke wangu alikuwa anampa 'housegirl' chupi zangu kunifulia, sikupenda!

Alisema mkewe hakuwa mtu wa kujukumika na ndio maana wakatengana.

Muhtasari

• Mkewe badala ya kumfulia, alikuwa anamwika mjakazi jukumu hilo.

Lukamba na aliyekuwa mke wake wa pili, Ceccy
Lukamba na aliyekuwa mke wake wa pili, Ceccy
Image: Instagram

Aliyekuwa mpiga picha rasmi wa Diamond Platnumz, Lukamba ambaye sasa ni msanii wa kujitegemea baada ya kuondoka WCB Wasafi amefunguka kwa mapana kilichosababisha uhusiano wake na aliyekuwa mpenzi wake Ceccy kuvunjika.

Akizungumza katika kipindi cha Lavidavi kwenye kituo cha Wasafi wakiwa na mpenzi wake mpya, Lukamba alisema kuwa mpenzi wake wa awali alikuwa mtu wa kuendekeza starehe sana kuliko kujukumika katika uhusiano wa ndoa.

Lukamba alivuka mipaka na kusema ya ndani kuwa kila siku walikuwa wanalumbana na Ceccy kwa vitu vidogovidogo kama kumfulia nguo.

Alisema Ceccy hakuwa anamfulia nguo, na kuwa hata zile za ndani alikuwa anampa dada mfanyikazi wa ndani kuzifua licha ya kuwa alikuwa mkewe na walikuwa wameshibana katika ndoa.

Sipendi mwanamke anayeendekeza starehe sana... napenda mwanamke anayejua majukumu yake kwa mwanaume, Ceccy alikuwa hanifulii nguo za ndani. Alikuwa anampa dada wa kazi afue, sikupenda hata kidogo na ndio maana tuliachana,” Lukamba alisema na kuibua mjadala mkali.

Kunao baadhi ambao walihisi alimuacha kwa vitu visivyofaa kwani mwanamke kukupenda si lazima kukufulia nguo za ndani huku wengine wakimpongeza kwa kumfukuza kwani kumpa mjakazi nguo za ndani za mpenzio kufua ni sawasawa na kumuonesha uchi wa mpenzi wako.

Gumzo kama hili liliibuka nchini Kenya wikendi iliyopita baada ya mchekeshaji Terrence Creative kusema kuwa alilazimika kurudia nguo ya ndani kutokana na uzembe wa kufua. Alisema mkewe Milly Chebby alisafiri kwa siku chache na akashindwa kufua nguo zake za ndani.

Je, ni sahihi mwanamke kumfulia mpenzi wake nguo za ndani?