'Nilikuwa nakunywa chupa 15 za bia Na silewi,'Weezdom afunguka kuhusu kupambana na msongo wa mawazo

Alisema mwaka huu umekuwa mgumu sana kwake.

Muhtasari
  • Kwa hivyo alizoea kunywa nyumbani kwake na angeweza hata kunywa chupa 15 za bia na asilewe kwa sababu alikuwa amezoea
Mwanamuziki Weezdom
Mwanamuziki Weezdom
Image: Hisani

Meneja wa zamani wa Bahati Weezdom katika mahojiano na Mwende Macharia kwenye kituo chake cha you,EMM, Weezdom alifunguka kuhusu yale ambayo amepitia.

Alisema mwaka huu umekuwa mgumu sana kwake.

Huu ndio mwaka ambao alikuwa ametambulisha wapenzi zaidi ya mmoja kwa umma na alisema kuwa hakuwa peke yake alipokuwa akifanya haya yote.

Weezdom alisema kuwa baada ya kuacha kazi na Bahati, maisha hayakuwa laini hivyo. Akiwa baba mtoto, alikuwa akituma pesa kwa ajili ya watoto wake na maisha yaliharibika, hakuweza kumudu pesa nyingi za kutuma na kulipa bili pia ikawa shida.

Alisema kwamba aliamua kuanza kunywa pombe na hakutaka mtu yeyote ajue anachopitia.

Kwa hivyo alizoea kunywa nyumbani kwake na angeweza hata kunywa chupa 15 za bia na asilewe kwa sababu alikuwa amezoea.

Wakati huu pia alichumbiana na wasichana wengi.

Mabadiliko yalitokea pale mbunge wa zamani Jaguar alipomtafutia kazi kama mbunge wa mwanasiasa fulani wakati wa kampeni na kwa sababu hakuweza kunywa pombe akiwa kwenye kazi ya aina hiyo na mfumo wake ulikuwa umezoea pombe, alipoteza fahamu.

Siku na dakika iliyofuata aliamka hospitalini. Baada ya utambuzi na matibabu, aliombwa kujiunga na kituo cha  lakini kwrehaba kuwa alikuwa ameamua mwenyewe kuacha pombe baada ya kupata fahamu, hakwenda kwenye rehab.