'Tulifungiwa hotelini,' Stevo Simple Boy afichua kwa nini hakutumbuiza katika shoo ya Mombasa

Msanii huyo aliwaomba mashabiki wake msamaha,huku akishukuru usimamizi wake kwa kusimama naye.

Muhtasari
  • Alifichua haya kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa alikataa kutumbuiza kwa sababu walikuwa wamefungiwa kwenye chumba cha hoteli

Msanii Stevo Simple Boy atokelezea na muonekano mpya
Msanii Stevo Simple Boy atokelezea na muonekano mpya
Image: Instagram

Mwimbaji  Stevo simple Boy amesimulia kuhusu hali ya kufadhaika aliyopitia alipokuwa Mombasa.

Msanii huyo mpya wa barida alipangiwa kutumbuiza katika mji wa pwani Jumatano usiku pamoja na  mwimbaji Ruger, Mcheshi Eric Omondi na mchezaji wa tik tok David Moya.

Alifichua haya kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa alikataa kutumbuiza kwa sababu walikuwa wamefungiwa kwenye chumba cha hoteli kwa sababu alikataa kutumbuiza bila kulipwa.

Alisimulia kwamba alishindwa kujitokeza baada ya waandaji wa hafla hiyo kushindwa kumlipa kabla ya kupanda jukwaani kufanya kama walivyokubaliana.

Stevo Simple Boy alisema aliumizwa na misukosuko aliyopitia lakini bado hatakata tamaa.Alionyesha upendo wake kwa Wakenya wanaounga mkono muziki wake.

"Ni kitu ambacho kimeniumiza kama msanii na kimenivunja moyo sana lakini bado sitakata tamaa. Bado nawapenda na kuwathamini wafuasi wangu wote. Tunajitahidi sana kama wasanii lakini ni Wakenya wenzetu. ambao wanajaribu kuchukua faida yetu," alisema.

Msanii huyo aliwaomba mashabiki wake msamaha,huku akishukuru usimamizi wake kwa kusimama naye.

"Naomba msamaha kwanza kwa mashabiki wangu na kushukuru management yangu @mibafrica mumejaribu Kadri wa uwezo wenu na mnapigania Sana kuniona juu kila wakati... Tunajaribu Sana kama wasani ila wakenya wenzetu ndo wanatudhulumu tulifungiwa hotelini @kiluaresort kwa sababu tumekataa kuperfom bila kulipwa na kampuni ya @sofire_fiesta Ni tendo ambalo limenifika kooni kama Msanii na imenikataa moyo Sana ila sikati tamaa kabisa ntazidii kupambana na nawapenda sana wakenya wanao ni support. Nashukuru Sana @loice_mwangi @vagagenius @gift_n_naima kwa kusimama na mimi huu wakati mgumu."