Uliniambia niseme "pochi" kwa video, ina maana gani? - Mamake Flaqo amuuliza

"Niliuliza Henry, nikakuuliza wewe na hata Sherly na hakuna mtu alinijibu" mamake Flaqo aliuliza.

Muhtasari

• "Hii pochi nasikia ikizungumziwa kila mahali ni nini?” mamake Flaqo almaarufu Mama Othis alifoka.

Flaqo akabiliwa na swali kuhusu pochi kutoka kwa mamake
Flaqo akabiliwa na swali kuhusu pochi kutoka kwa mamake
Image: Instagram

Mchekeshaji Flaqo amejipata pabaya baada ya mamake kumkaripia kwa swali la kutaka kujua maana na neno ‘pochi’ ambalo msanii huyo alimwambia mamake kutaja kwenye moja ya skits zake.

Msanii huyo alipakia picha ya mazungumzo yake na mamake akimzomea na kutaka majibu bada ya kugundua kuwa huneda neno hilo lina maana fiche kutokana na jinsi watoto wengine walikuwa wanajikunyata kwa aibu alipokuwa akitaka kujua maana ya pochi kutoka kwao.

“Na hii video umepakia leo hilo neno “pochi” unaniambia niseme kwa video lina maana gani? Niliuliza Henry, nikakuuliza wewe na hata Sherly na hakuna mtu alinijibu. Hii pochi nasikia ikizungumziwa kila mahali ni nini?” mamake Flaqo almaarufu Mama Othis alifoka kwenye mazungumzo hayo ya WhatsApp.

Kwa kuanzia, neno Pochi linatokana na mfumo wa malipo ya pesa kupitia miamala ya kidijitali. Mfumo huu kwa jina ‘Pochi la biashara’ ulizinduliwa na kampuni husika ili kuwezesha wafanyibiashara kutenganisha malipo ya kibiashara ya kidijitali kutoka kwa malipo mengine.

Lakini nchini Kenya katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na memes ambazo zimekuwa zikisambazwa na vijana zilitumia neno “pochi” kutoka kwa muktadha huo kwa njia hasi.

Kulingana na memes nyingi ambazo zimekuwa ziizua utani kuhusu neno “pochi” – maana nyepesi wanajaribu kuelezea watu haswa wanadada ambao wanatoa rushwa ya ngono ili kupata faida fulani.