Mtoto wa Rais Ruto Nick na mkewe wakimkaribisha mtoto wao wa kwanza (Maelezo)

Nick alimuoa Chemtai, katika sherehe nzuri ya kitamaduni mnamo Januari 2022.

Muhtasari

• Nick, ambaye kitaaluma ni wakili, alimuoa Chemtai, katika sherehe nzuri ya kitamaduni mnamo Januari 2022 kulingana na desturi za Kalenjin.

• Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga alimpa Nick idhini ya kujiunga na baa hiyo mwaka wa 2019.

Nick Ruto na mpenzi wake Chemutai
Nick Ruto na mpenzi wake Chemutai
Image: Maktaba

Rais William Ruto na mkewe Rachel Ruto wanajivunia kuitwa babu na bibi baada ya mtoto wao Nick Ruto na mkewe Evelyn Chemutai kupata mtoto wao wa kwanza.

Mkuu wa Nchi alifunguka habari hizo njema siku ya Jumapili, wakati wa Ibada ya Kanisa huko Nanyuki.

"Mwaka jana, tulikuja hapa kulipa mahari na sasa nataka kuwashukuru wenyeji wa Laikipia, ambao walimpa mwanangu mke, kwa sababu tumejaliwa mjukuu," alisema Rais Ruto.

“Pengine kuwa kwangu hapa mapema kunahusiana na hilo! Kwa hivyo asante kwa watu wa Laikipia kwa kutoa kuwa binti-mkwe. Familia yetu inakua,” aliongeza.

Nick, ambaye kitaaluma ni wakili, alimuoa Chemtai, katika sherehe nzuri ya kitamaduni mnamo Januari 2022 kulingana na mila za Kalenjin.

Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga alimpa Nick idhini ya kujiunga na baa hiyo mwaka wa 2019 kama Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya.

Mnamo 1991, Rais Ruto alifunga ndoa na Rachel, na wawili hao wakaenda kupata watoto saba pamoja.

Watoto wengine wa Rais Ruto ni June Ruto, Charlene Ruto, Stephanie, Cullie, George na Nadia.