Choffuri: Mpenzi wangu hawezi niacha, nyanyangu amenipa hirizi ya kushikilia uhusiano

Choffuri alisema kuwa watu wenye pesa wamejaribu kumtongoza Nekesa lakini wameshindwa kufaulu kutokana na nguvu za 'kitu' kutoka kwa nyanya yake.

Muhtasari

• Khalayi na Choffuri wamekuwa na mahusiano ya kuachana na kurudiana kwa muda na alisema kuwa hawezi muacha hata kama ni mkubwa kiumri kumliko.

• Mimi huwa naenda kwa nyanya yangu ananipatia kitu kidogo, naweka na inashikilia uhusiano, kwa hiyo inakuwa ni kusukuma tu - Choffuri.

Choffuri azungumza kinachodumisha uhusiano wake na mpenzi wake
Choffuri azungumza kinachodumisha uhusiano wake na mpenzi wake
Image: Facebook

Mchekeshaji Choffuri amefichua kile ambacho kilifanya akarudiana na mpeniz wake, mwanamuziki Nekesa Khalayi.

Nekesa na Choffuri waliachana miezi kadhaa na mnamo mwezi Septemba, mchekeshaji huyo aliapa kwa utani kuwa angemrudisha mpenzi wake na kuendelea kwa mahaba yao.

Katika kile ambacho wengi walidhani ni mzaha, Choffuri alifanikiwa kurudiana na Khalayi na sasa amefichua kile ambacho kinadumisha mapenzi yao licha ya kuwepo kwa changamoto kibao.

Choffuri anasema kuwa na Khalayi hakujakuwa rahisi kwa vile kuna watu wengi wenye pesa ambao wanamtamani na kumtolea macho lakini amefanikiwa kumweka kwake kwa kile alisema kuwa ni usaidizi wa nyanya yake.

“Waheshimiwa wanamtaka, na unajua wao wako na kitu kidogo, na hiyo unajua ni changamoto yeye kurudi kwa nyumba. Lakini tuko tu. Mimi huwa naenda kwa nyanya yangu ananipatia kitu kidogo, naweka na inashikilia uhusiano, kwa hiyo inakuwa ni kusukuma tu,” alisema.

Mchekeshaji huyo alisema katika uhusiano wake na Khalayi, wameachana na kurudiana kwa mara kadhaa lakini ‘kitu kidogo’ kutoka kwa Nyanya yake kimekuwa kikimsaidia sana katika kudumisha uhusiano huo.

Mwezi mmoja uliopita, Choffuri alidokeza kuwa Khalayi ni mkubwa kiumri kumliko na kusema anamwita mama na kuwaambia wambea wake kuwa katu hayuko tayari kumuacha leo wala kesho.

“Huwa namwita mama kwa sababu yeye ni mkubwa kuliko mimi na ninaamini mama wote ni bora na upendo wa kweli ️Nekesa khalayi,” Choffuri alisema huku akisukuma wimbo mpya kipindi hicho kwenye YouTube kwa jina Romeo Khalinjola.