Willy Paul amuomba Diamond kufanya 'challenge' ya wimbo wake mpya

Pozee alimsifia kwa kusema kuwa yeye ndiye Simba wa muziki wa Afrika Mashariki.

Muhtasari

• Pozee amekuwa akiupigia debe wimbo huo kwa kusema kuwa ulimgharimu zaidi ya milioni mbili kwa video yake.

Pozee amtaka Mond kufanya challenge ya wimbo wake
Pozee amtaka Mond kufanya challenge ya wimbo wake
Image: INSTAGRAM

Msanii wa kizazi kipya nchini Willy Paul ametoa ombi la hakika kwa mwenzake kutoka Tanzania Diamond Platnumz kumfanyia heshima na kushiriki video akifanya igizo cha wimbo wake mpya kwa jina Umeme.

Pozee, kama anavyojiita alipakia video fupi akidensi kwa wimbo huo wake na kumuomba Diamond kufuata jinsi alikuwa anasakata densi ili kufanya ‘challenge’ moja ya wimbo huo kama njia moja ya kumpa shavu katika kufikia watu wengi kwa ajili ya wimbo huo aliouachia siku nne zilizopita.

“Diamond Pltnuzm tafadhali nipigie challenge moja kaka. Fuata tu jinsi ninavyocheza densi hapo na natumai utaipenda jinsi nilizika kabisa,” Willy Paul alisema.

Alizidi kumtongoza Diamond kwa kumvika koja la maua yake kuwa yeye ndiye simba wa muziki wa Afrika Mashariki na kumtaka kushirikiana naye ili kupeleka muziki wa kanda hii mbele zaidi.

“Yaani nimeua tu #umemechallenge ama vipi? Afrika Mashariki Simba ni wawili tu Mimi na Wewe kaka.. tupeleke muziki wa Afrika Mashariki mbele zaidi,” Willy Pozee alisema.

Msanii huyo amekuwa akiupigia wimbo wake mpya debe kwa kuupaisha kuwa umemlazimu kuzama kwa kina kikubwa mfukoni.

Alisema kuwa ili kufanikisha sauti tu, alitumia zaidi ya laki 5 na video yenyewe ilimgharimu zaidi ya milioni mbili pesa za benki kuu ya Kenya.

Inasubiriwa kuonwa kama Diamond ataitikia ombi la Pozee na kufanya challenge akidensia huo wimbo au atabeza.

Wakenya wengi huwa wanakumbatia ngoma za wasanii kutoka Tanzania na kufanya challenge zao, akiwemo Eric Omondi ambaye mwishoni mwa mwaka jana alifanya challenge ya Chitaki ya Diamond na kupata kashfa nyingi.

Omondi alitupiwa maneno kwa kuwa amekuwa katika mstari wa mbele akishtumu miziki ya kigeni kutawala humu nchini lakini katika video hiyo akaonekana kuwa ndiye anaisukuma kwa kufanya challenge.