Betty Kyallo adokeza kupata mwanamume, "Siko peke yangu, namficha kama bangi"

“Safari hii NAMFICHA kama bangi... Ni 2023....Labda ata ni Bodyguard wangu na Hamumjui.... " - Kyallo.

Muhtasari

• Kyallo aliachana na Nick Ndeda takribani mwaka mmoja uliopita na alisema hakuwa tayari kwa mapenzi tena.

Betty Kyallo adokeza kuwa katika uhusiano
Betty Kyallo adokeza kuwa katika uhusiano
Image: Instagram

Mwanahabari Betty Kyallo amefichua kuwa ana mwanamume ambaye wanachumbiana naye mwaka huu wa 2023.

Betty katika mahojiano kwa njia ya simu na kituo kimoja cha redio humu nchini alisema kuwa hawezi kaa peke yake huku akikataa kabisa kumzungumzia mwanaume huyo wake na kusema hatoweka jina lake wazi.

Mwanahabari huyo alizua mzaha alipoulizwa kutoa maelezo zaidi na kusema kuwa “acha nikate simu kabla niachwe!”

Kyallo alisema kuwa watu hawawezi kumjua huyo mpenzi wake kwa urahisi, akidokeza kuwa pengine wanaweza kuwa wanamuona bouncer akimpa ulinzi kumbe ndio mtu wake.

“Safari hii NAMFICHA kama bangi... Ni 2023....Labda ata ni Bodyguard wangu na Hamumjui.... " Kyallo alisema kwa utani.

Haya yalijiri saa chache baada ya watu wasiojulikana kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kuwa picha zake chafu zimevujishwa

Kupitia kwa kampuni inayosimamia kazi zake ya Medios, Kyallo alitoa tamko kali dhidi ya uvumi huo na kudokeza kuwa tayari suala hilo lilikuwa limevaliwa njuga na maafisa wa ujasusi DCI ili kumtia nguvuni yule ambaye alikuwa anajaribu kumchafulia jina.

Tangu kuachana na Nick Ndeda takribani mwaka mmoja uliopita, mwanahabari huyo hajawahi kuonekana au hata kusikika hadharani kama anachumbiana na mwanamume mwingine mpaka alipodokeza katika mahojiano hayo.

Betty waliachana na wakili Nick Ndeda baada ya kuchumbiana kwa muda mfupi na alisema kuwa angechukua likizo ndefu kutoka kwa jungu la mapenzi ili kujiboresha kimaisha na pia kupata muda wa kuangazia maisha yake pamoja na ya mwanawe.