Chris Kirwa awazima wanaomkejeli Trio Mio baada ya matokeo ya KCSE

"Nyi wote mngekuwa na A mngekuwa ma civil engineer, mnapigania kuget position mtoi wa mkuu anaorganiziwa,".

Muhtasari
  • Juzi tu, Trio alisema hana wasiwasi kuhusu alama atakayopata mara tu matokeo ya Cheti cha Elimu ya Sekondari (KCSE) yatakapotangazwa
Image: INSTAGRAM// TRIO MIO

Rapa  Trio Mio kwa sasa anavuma katika nambari moja kwenye Twitter baada ya Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu kutangaza matokeo ya KCSE ya mwaka wa 2022.

Wakenya kwenye Twitter (KOT), walimfanya nyota huyo chipukizi kuwa mada inayovuma huku wakingoja kwa hamu kuona atapata matokeo gani katika mitihani ya KCSE.

Juzi tu, Trio alisema hana wasiwasi kuhusu alama atakayopata mara tu matokeo ya Cheti cha Elimu ya Sekondari (KCSE) yatakapotangazwa.

‘’Dimba sijawaikuwa timu ya kuanzia, mbuku sishiki nothing in, but kitu inaitwa mziki mimi ni mwalimu mkuu na marking scheme,” anaimba kwenye video ya dakika 2.

“Ka topic ni success niko na A kwa school of life, ile KNEC watanipea haitawai kuamua chakula changu…”

Anaendelea kuimba;

"Nyi wote mngekuwa na A mngekuwa ma civil engineer, mnapigania kuget position mtoi wa mkuu anaorganiziwa,".

Watahiniwa 1,146 kati ya 881,416 waliofanya mitihani ya KCSE 2022 walipata A alama ya A.

Huku Kirwa akizungumzia kejeli abazo msanii huyo amepokea kutoka kwa Wakenya amesema;

"Kwa wale wanaomkejeli Trio kwa matokeo yoyote aliyopata: Hapata alama ya A , hatabebwa bega juu, vichwa vya habari havitapiga kelele jina lake kama mwanafunzi bora! Lakini baada ya miaka michache ataajiri Wanafunzi bora kama wasimamizi wake - Soon Bro !💪"