Jux hataki kupima 'kipimo kikubwa' ili kuzaliwa mtoto na mpenzi mpya - Mwijaku adai

Mwijaku alisema kuwa mpenzi mpya wa Jux anadai wafanye vipimo vikubwa kwanza ili amzalie lakini msanii huyo hayuko tayari.

Muhtasari

• Wengi walimtaka Mwijau kufanya ufafanuzi zaidi maana ya kipimo kikubwa.

Mwijaku aibua makubwa kuhusu Jux na mpenzi wake mpya
Mwijaku aibua makubwa kuhusu Jux na mpenzi wake mpya
Image: Instagram

Mwishoni mwa wiki jana, msanii Juma Jux aliweka wazi picha yake akiwa na mpenzi wake mpya ambaye wengi walihisi anashabihiana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, mtangzaji na mwanamuziki Vanessa Mdee.

Sasa mapya yameibuka kutoka kwa mtangazaji mbwatukaji Mwijaku Burton ambaye amesema alikuwa na mazungumzo na msanii huyo kuhusu hatima ya uhusiano wao.

Jux tangu kuachana na Vanessa, amekuwa mkimya na msiri wa kutoonyesha hadharani maisha yake ya kimapenzi na muda wote amekuwa akisukuma sana biashara zake za duka la nguo la muziki.

Kulingana na Mwijkau, tayari amekuwa na mazungumzo na Jux na kufichuliwa kuwa mpenzi mpya wake ako tayari kumbebea ujauzito na kumzalia kwa sharti moja.

Mwijaku alisema kuwa Jux alitakiwa kufanya vipimo ‘vikubwa’ ili kuzaliwa, jambo ambalo Jux anadaiwa kutokuwa tayari kutekeleza. Hata hivyo aliwaacha wengi kwenye mataa wasijue ‘kipimo kikubwa’ kina maana gani haswa.

“Nimeongea na JUX leo amenambia mpenzi wake mpya yupo tayari kuzaa naye ila amesisitiza kupima kipimo kikubwa kabla hajaafiki kubeba ujauzito wa jux . Na jux hayupo tayari kupima kipimo kikubwa,” Mwijaku alisema.

Wengi walijijazia kuhusu ‘kipimo kikubwa’ wakisema kuwa huenda ni vipimo vya virusi vya HIV huku pia wengine wakikisia kuwa alikuwa na maana ya kupima uzazi ili kudhibitisha ikiwa ana uwezo wa kuzalisha.

Ikumbukwe msanii huyo mwenye fasheni ya kipekee alikaa na Vanessa Mdee kwa muda mrefu ila hawakuweza kubarikiwa na mtoto, lakini Mdee alivyokwenda zake Marekani na kuolewa na msanii Rotimi, haikuwachukua muda kabla ya kutangaza habari za ujauzito wao wa kwanza.

Kutokana na hili, wengi wamekuwa wakizua uvumi wa chini ya zulia kuwa huenda Jux ndiye alikuwa mwenye tatizo jambo ambalo pengine ndilo lilisababisha uhusiano wao kuvunjika.

Si Jux wala Vanessa ambaye amewahi jitokeza hadharani na kuzungumzia kilichokwamisha uhusiano wao.