Hisia mseto baada ya Embarambamba kuachia kibao cha kumuenzi Magoha

Viongozi,wanasiasa na Wakenya wanaendelea kutuma risala za rambirambi kwa familia ya mwendazake.

Muhtasari
  • Huku wakenya wakiendelea kutuma risala zao kwa familia ya marehemu Magoha, mwanamuziki wa nyimbo za injili Embarambamba ametoa wimbo mkali wa kumuenzi marehemu profesa
Image: INSTAGRAM// EMBARAMBAMBA

Msanii wa nyimbo za injili Embrambamba amejipate upande mbaya na Wakenya baada ya kutoa kibao cha aliyekuwa waziri wa Elimu George Magoha.

Magoha aliaga dunia siku ya Jumanne baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.

Viongozi,wanasiasa na Wakenya wanaendelea kutuma risala za rambirambi kwa familia ya mwendazake.

Huku wakenya wakiendelea kutuma risala zao kwa familia ya marehemu Magoha, mwanamuziki wa nyimbo za injili Embarambamba ametoa wimbo mkali wa kumuenzi marehemu profesa.

Wimbo huo ambao umetoka tu siku moja baada ya kifo cha Prof umewaacha Wakenya wengi wakitoa hisia tofauti mitandaoni.

โ€œWacha kunyamaza hivyo George Magoha,โ€ Ameimba Embarambamba.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wanamitandao;

Ripped Jeans: Kumbe ata wazimu hujua where to draw the line? I thought angepull moja kali aruke huko ndani smh!

Georgina Njenga: Si tulisena government ifence kisii na iuzwe๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ

El Njeve: Man busy shaming us all๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Albert KIbiwott: We are tolerating nonsense too much

All fun: We are tolerating nonsense too much