Mchekeshaji Nasra Yusuff ammezea mate msanii Bien, asema yeye ni mpenzi wake

Mchekeshaji huyo walitengana na aliyekuwa mpenzi wake Rashid mwishoni mwa Novemba mwaka jana.

Muhtasari

• Nasra akitangaza kuachana na mpenzi wake, alisema alijaribu kupigania uhusiano huo lakini maji yaliziki unga.

Nasra Yusuf
Image: Nasra Yusuf

Mchekeshaji wa shoo ya Chruchill, Nasra Yusuff amejitokeza kuonesha waziwazi jinsi anavyommezea mate msanii wa Sauti Sol, Bien Aime Baraza.

Yusuff ambaye alipoteza ndoa yake miezi michache iliyopita aliingia kwenye instastory yake na kuachia maneno ya kumtamani Bien huku akifunguka bila woga kwamba yeye ni mke wa msanii huyo.

“Na huyu Bien anajua kwamba mimi ni mke wake kweli,” mchekeshaji Nasra aliandika.

Itakumbukwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana Nasra aliweka wazi kwamba yeye na aliyekuwa mume wake Director Rashid hawakuwa tena pamoja, miezi kadhaa baada ya wawili hao kutangaza kuharibikiwa na ujauzito.

Akitangaza kuachana na Rashid, Nasra alisimulia katika chapisho refu jinsi alijitoa kwa hali na mali kupigania uhusiano wao lakini aliishiwa na pumzi.

“Kwa hivyo ndio niko peke yangu….yeyote anayenijua anajua kuwa nimepigania uhusiano huo. Nilipoteza mawasiliano ya familia kwa sababu yake, nilijipoteza na kazi yangu nilipoteza marafiki kwa sababu yake, nilipata ukosoaji wa mara kwa mara kutoka kwa jamii yangu kwa sababu yake lakini bado nilikuwa tayari kuifanya ifanyike ingawa mizizi ya shida zetu ilikuwa kila mwaka kwa miaka 5,” Nasra alisimulia kwa sehhemu.

Nasra ambaye mpaka sasa hajaweka wazi kama anaonana na mwanamume mwingine sasa amejitokeza wazi kusema kwamba yeye ni mrembo wa Bien hata kama msanii huyo bado hajatambua hilo.

Wikendi iliyopita, Bien aligonga vichwa vya habari baada ya mkewe Chiki Kuruka kumkaripia mwanamke aliyejaribu kutingisha makalio yake jukwaani nyuma ya mumewe Bien.

Chiki alifika kwa haraka jukwaani na kumfukuza mwanadada yule, hatua ambayo baadae Bien aliitetea huku akisema kwamab si wivu bali ni hali ya kazi.

Bien aliweka wazi kwamba mkewe ndiye meneja wake na kumfukuza yule mwanadada iikuwa njia moja ya kumwekea mumewe mazingira rafiki ili kutumbuiza jukwaani.