Zuwena ya Diamond ilirekodiwa miaka 4 iliyopita - Meneja wake, Babu Tale

Tale alisema kuwa bado kuna ngoma zingine zitatoka mwaka huu za Diamond zilizorekodiwa miaka 7 iliyopita.

Muhtasari

• Msanii Diamond alitoa ahadi kwa mashabiki wake kuwa huu ndio mwaka angewaporomoshea ngoma kwa mfuluizo, tayari hilo limeonekana,.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Meneja wa Diamond Platnumz, ambaye pia ni mbunge Babu Tale amefunguka za ndani kuhusu wimbo mpya wa msanii huyo. Kulingana na Babu Tale, wimbo wa Zuwena ambao unazidi kutamba kwenye mawimbi kwa siku ya tano sasa haujarekodiwa mwaka huu kama ambavyo wengi wanahisi.

Japo wimbo huo umetolewa wiki hii, lakini Tale alifichua kwamba Diamond Platnumz alirekodi wimbo huo miaka mine iliyopita ila akauweka kibindoni bila kuutoa.

Tale alisema pamoja na mameneja wenzake kama Sallam SK na mkubwa Fella waliusikiliza sana na kumtaka Diamond akubali wimbo utoke ila akakataa akisema kuwa muda wake haukuwa umefika.

Kinginge ambacho hamkijui kwenye huu wimbo #Zuwena nikwamba umerekodiwa miaka minne (4) iliopita yaani mimi na wenzangu @mkubwafellatmk @sallam_sk tumeusikiliza mpk tukaukatia tamaa kuwa hautatoka... niliwahi kumtafuta @lamataleah awe Muongozaji wa huu wimbo na alikua tayari.. tatizo lilikuwa kwa mwanamziki mwenyewe alidai muda wa huu wimbo kutoka bado.. na ikiwa tayari nitakwambia Boss..” Babu Tale alisimulia.

Baada ya kukata tamaa kuwa huenda Diamond hakufurahishwa na utunzi wa ule wimbo miaka 4 iliyopita, ghafla alipata ujumbe kutoka kwake akimwambia kuwa muda kamili wa kuachia dude la miaka 4 ndio mwaka huu.

Tale alisema waliingiwa na wasiwasi kuwa huenda maudhui yake yatakuwa yamezeeka na hautapokelewa vizuri lakini kwa mshangao, wimbo huo umepata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wake na kuufanya gumzo la mijini na vijijini kote Afrika mashariki.

Basi mwezi mmoja nyuma kanambia huu ndio mwaka wa ZUWENA kutoka na nitaidirect mwenyewe... niliogopa kwa kuwa niliona wimbo umekaa sana ndani...ni kweli utafika Kule tunapotaka ufike? Ghafla wimbo umefika na umekua mkubwa Africa.. Kuna cha kujifunza hapa.. KIZURI NI KIZURI TU HATA UKIFUNIKE NA GUNIA.. niwaibie siri..bado zingine mbili nazo zilirekodiwa miaka saba (7) iliopita naamini zitapokelewa vizuri pia,” Tale alimwaga mtama.