Usijaribu mtumishi wa Mungu-Sonko aambiwa baada ya kumsihi muhubiri Owuor haya

Pia amesema kwamba baada ya kumponya mbunge huyo atatubu dhambi zake zote.

Muhtasari
  • Sonko aliandika ujumbe huo huku ukiwa umeambatinishwa na picha ya muhubiri huyo akiwa amebeba magongo

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ameonywa na mshabiki wake dhidi ya kumjaribu muhubiri Owuor.

Hii ni baada ya Sonko kumsihi muhubiri huyo aweze kumponya mbunge wa EALA  Sankok.

Sonko aliandika ujumbe huo huku ukiwa umeambatinishwa na picha ya muhubiri huyo akiwa amebeba magongo baada ya kuwaponya watu waliokuwa wakitumia magongo hayo.

Pia amesema kwamba baada ya kumponya mbunge huyo atatubu dhambi zake zote.

Ujumbe wake ulisoma;

"Hii ni miujiza mikubwa. Kuna Mungu mbinguni anayeponya. Ombi langu rahisi la unyenyekevu kwa Mtume wetu mpendwa Owuor anaweza pia kufanya muujiza kwa ndugu yetu Mhe. David Ole Sanok Mbunge wa EALA basi ikiwa atapona nitaenda kwa nabii moja kwa moja nitubu dhambi zangu zote na kuokolewa ili kuwa Mkristo aliyezaliwa mara ya pili. Sote tuombe muujiza huu mkubwa utendeke."

Wanamitandao na mashabiki walitoa hisia mbalimbali na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

Osborn ambani: Usijaribu mtumishi wa Mungu πŸ˜‚πŸ˜‚

B.Karei ALI : Wakkshana na prophet kabsaa ongelea uhuru mwenye umezoea , then bangi should remain burned 🀣🀣

Kiprotich Robert: Mike Sonko. Sonko BwanaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚hata mimi nategea hio miracle

Erick Mogeka: You remember when Jesus was in the wilderness after being baptized.. satan took very simple temptations to him..kama hizi tu