Hisia mseto baada ya mhubiri Ezekiel kudai hakuna mwanamke mwenye dreadlock amewahi kuwa katika mahusiano mazito

Muhtasari
  • Kulingana na ripoti zilizotolewa na Wakenya wengi, walidai kuwa inasikitisha sana kwamba Mhubiri huyo maarufu anawasuta Wakenya wenye dreadlocks

Mchungaji maarufu wa Kenya Ezekiel Odero amesema kuwa hakuna mwanamke mwenye dreadlocks ambaye amewahi kuwa katika mahusiano mazito.

Katika taarifa ya habari ambayo imesambaa mitandaoni imefichuka kuwa mchungaji Ezekiel amedai kuwa ni bahati mbaya sana kwamba vijana wengi bado hawajaamini.

Mhubiri huyo mashuhuri kwa muda amevutia hisia za vijana juu ya matamshi yake.

Huku wakijibu matamshi yake, Wakenya waliotumia akaunti zao tofauti za mitandao ya kijamii kutoa maoni yao kuhusu suala hilo wamemtaka Mhubiri huyo mashuhuri kuelewa kwamba hii imekuwa mtindo.

Kulingana na ripoti zilizotolewa na Wakenya wengi, walidai kuwa inasikitisha sana kwamba Mhubiri huyo maarufu anawasuta Wakenya wenye dreadlocks ingawa baadhi ya watu wenye dreadlocks wanafanya hivyo kwa mila.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wanamitandao baada ya  matamshi ya mhubiri huyo;

Daisy Njoki: Ndio maana huwa nauliza Mungu kwanza kabla ya kujiunga na kanisa lolote,nafurahi kwa maana  nahudumiwa na nguvu za Mungu

Akeshi Kunga: Oooi ma.๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ..ninapokumbuka kusoma biblia yako ni bure na cheka.

Esther Thathi Rastagal:  aki bona wana tuonea na ss ndio tuko ๐Ÿ•บ๐Ÿ•บ

Sly Wanjiku Sylvia:  nipeleke kinyozi siezi kaa bila nyota

Grace Nyawira Gichira: Aacha uongoo hubiri maadili ya ndoa takatifu ya MUNGU watu wengine waache kusema umalaya ni ndoa ya wake wengi na unjue mbinguni ni mbali mhubiri

Faith Gichuru:  dreadlocks are the best for African hair. I stopped braiding and perming my hair along time ago. If I attend his service I shall not and will never cut my locks.