Familia ya Diamond wafurahia wimbo wa Harmonize hadharani, wajitenga na ugomvi wao

Binamu ya Diamond Romy Jones na dadake Esma Platnumz kila mmoja alipakia video akicheza wimbo wa Harmonize, Single Again.

Muhtasari

• Harmonize na Diamond hawajakuwa na amani baina yao tangu kuondoka kwake WCB Wasafi mwaka 2019.

Harmonize afurahia familia ya Diamond kucheza muziki wake
Harmonize afurahia familia ya Diamond kucheza muziki wake
Image: Screengrab

Romy Jones au RJ the DJ, binamu wa Diamond Platnumz ambaye pia ni mcheza santuri rasmi wa msanii huyo amefanya kitendo amabcho kimeibua gumzo pevu kwentye mitandao ya kijamii.

RJ wikendi iliyopita alikuwa anapakua burudani kwenye kilabu moja ambapo akiwa shughulini alionekana akiufurahia wimbo wa Harmonize, Single Again.

Kuonekana akifurahia na kuucheza wimbo wa Harmonize kulikuwa gumzo kubwa kutokana na dhana ambayo kwa takribani miaka 4 imekuwepo kwamba tangu Harmonize kuondoka WCB Wasafi, hakuna Amani kati yake na kila mtu aliyebaki kwenye lebo hiyo inayoongozwa na Diamond Platnumz.

Harmonize aliondoka mwaka 2019 kwa kishari mno akivunja uhusiano na watu wengi katika lebo ya Wasafi wakiwemo waliokuwa wasanii wenza pamoja na wafanyikazi wengine, katika kile ambacho kilitajwa kuwa ni agizo kutoka kwa Diamond ambaye hakupendezwa na kuondoka kwa msanii huyo aliyekuwa akipiga riziki ndefu kwa faida ya lebo hiyo.

Lakini kitendo cha binamu wa Diamond kucheza ngoma ya mbaya wa bosi wake kwenye kilabu si kigeni kwani hivi majuzi pia dadake Diamond, Esma Platnumz alipakia video akifurahia wimbo wa Harmonize akiwa ndani ya gari, video ambayo Harmonize vile vile aliipakia kwenye Instagram yake.

Hii ni ishara kubwa kwamba familia ya Diamond imejitenga mbali na matatizo au ugomvi baina ya wasanii hao ambao walikuwa marafiki wakubwa miaka michache iliyopita.

Wengine walitabiri kwamba hawa ni watu ambao Diamond amewatumia ili kujaribu kurekebisha uhusiano wake na Harmonize na pengine siku za mbeleni huenda watajirudi na kufanya kazi pamoja tena.