Nimewahata-Mejja asema baada ya kupewa ruhusa ya kurejea kuimba na daktari

Mwimbaji huyo mashuhuri pia alipaswa kwenda kupata matibabu ya usafi wa sauti ili apone kikamilifu.

Muhtasari
  • Ufichuzi wa Mejja hata hivyo unakuja siku chache baada ya kutangaza kwa mashabiki wake kwamba alikuwa akipumzika kutoka kwa muziki
Mejja Genge

Mwimbaji mashuhuri wa Kenya Meja Khadija almaarufu Mejja leo ametangaza kwa mashabiki wake kwamba amepewa ruhusa na daktari wake kurejea kufanya muziki wake tena.

Hii ilikuwa kupitia chapisho la hivi punde kwenye akaunti yake ya Instagram, ambapo alifichua kuwa daktari wake alikuwa amemwagiza zaidi kufanya muziki huo lakini kwa tahadhari fulani.

Mejja alishiriki kipande cha video fupi ambapo alikuwa na daktari wake hospitalini, na akaisindikiza na maandishi yanayosema;

"Nimepewa Greenlight Na My Dr. Finally Back To Work But With Caution" Mejja aliandika.

Mejja uptia kwenye ukurasa wake wa instagram pia amewaambia mashabiki wake kuwa alikuwa amewapeza, huku akisema kwamba ugonjwa wake umemfanya ajifunze mengi.

"Back To Basics!!!! NiMewahata Manze TuPaTaNe Marima, I Have Learned A lot Through This Process About Patience Na Pia Who Your Real Friends Are TuBaki Hivo Hivo MPAKA sahii Uzito Wagenge JAHBLESS."

Ufichuzi wa Mejja hata hivyo unakuja siku chache baada ya kutangaza kwa mashabiki wake kwamba alikuwa akipumzika kutoka kwa muziki.

Alitoa tangazo hilo mapema mwezi huu, na hii ni kwa sababu alikuwa akikabiliwa na matatizo ya koo na daktari wake alikuwa amemshauri kufanya hivyo.

Mwimbaji huyo mashuhuri pia alipaswa kwenda kupata matibabu ya usafi wa sauti ili apone kikamilifu.

Katika mahojiano na mtangazaji wa redio Willy M Tuva, Mejja alifichua kuwa alikuwa akipata virutubisho ili kutibu matatizo ya koo aliyokuwa nayo.